Foleni ya pikipiki zikisubiri kupata huduma ya nishati ya mafuta ambayo imeadimika kiasi kikubwa mkoa Mbeya hivi sasa.
Kutokana na tatizo la kuadimika kiasi kikubwa kwa mafuta, baadhi ya vijana wamepata ajira isiyo rasmi kwa kununua mafuta hayo vituoni na kwenda kuyauza kwa wahitaji. Petroli wanauza sh. 5,000 kwa lita moja. Vijana hawa hupanga foleni na hata kulala vituoni wakisubiri huduma hiyo, pichani wakionekana kuchoka na hata kulala kituoni hapo kusubiri kupata mafuta na kwenda kuyauza kwa bei ya juu.
Bei halisi ya mafuta ni hiyo lakini sasa walanguzi bei imepanda kwa aina ya mafuta ya petrol lita moja kwa sh. 5,000 mpaka sh 6000 kwa lita moja
Foleni kituo cha mafuta
Picha zote na mbeyayetu.blogspot.com