Hakuna wa Kumzuia Yanga, Waangola Waona Cha Moto Taifa

yanga

Kweli Yanga sasa ni zaidi ya Moto wa Petroli, imefanikiwa kuisambaratisha Timu ya Esparance ya Angola kwa Mabao 2 -0 katika hatua ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika

Magoli ya Yanga yamefungwa na Simon Msuva pamoja na Matheo Anthony na kuiweka yanga kwenye mazingira mazuri ya kufuzu kucheza hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Simon Msuva alianza kuifungia Yanga bao dakika ya 71 kipindi cha pili kwa kuunganisha kwa kichwa krosi ya Geofrey Mwashiuya kabla ya kabla ya Matheo kuipa Yanga bao la pili dakika za nyongeza kwa shuti kali akiwa nje ya takribani mita 25 kutoka golini.