SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua mwamuzi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Hafidh Ali kuwa Kamishna wa mechi kati ya El Ahly Shandy na Al Hilal zote za Sudan.
Shandy ndiyo mwenyeji wa mechi hiyo namba 98 ya Kombe la Shirikisho itafanyika Agosti 5 mwaka huu na itachezwa Uwanja wa Shandy ulioko katika mji wa Shandy.
Mwamuzi wa mechi hiyo ni Raj Seechun kutoka Mauritius ambaye atasaidiwa na Balkrishna Bootun, Jean Daniel Telvar na Parmendra Nunkoo, wote pia kutoka Mauritius. Mratibu Mkuu wa mechi hiyo ni Paul Bassey wa Nigeria.