Kuhusu TheHabari

Karibuni sana wadau hapa dev.kisakuzi.com!

Shukrani kwa kuperuzi kurasa zetu, ambazo zimesheheni habari mbalimbali za kusisimua, kufurahisha, kuonya na kuelimisha. Kwa heshima na taadhima, tunapenda kukujulisha kuwa baadhi ya Watanzania wadau wa habari waishio Los Angeles, California, kwa kushirikiana na wenzetu wa nchini Tanzania tunaendesha mtandao huu kwa ajili yako Mtanzania popote ulipo. Kama tujuavyo nchi yetu inatumia lugha kuu mbili, yaani Kiswahili na Kiingereza. Kwa mantiki hiyo, lugha hizi mbili ndizo zitakazotumika kupashana habari hapa, ingawa Kiswahili kitapewa kipaumbele zaidi katika lengo zima la kuchangia na kuunga mkono ukuaji wake.

TheHabari.com ni mtandao wa kizalendo unaokuletea habari za kijamii, kisiasa, burudani, na teknolojia. Hii ni kwa kushirikiana na Watanzania wenzetu popote walipo duniani katika kuelimishana na kufahamishana mustakabali mzima wa nchi yetu. Tumedhamiria kuleta habari kwa uwazi na umakini bila uwoga wala upendeleo wa aina yeyote. dev.kisakuzi.com haifungamani na upande wowote zaidi ya maslahi ya Tanzania na watu wake. Hivyo basi tushirikiane katika kuendeleza gurudumu la maendeleo katika nchi yetu tuipendayo Tanzania.

Tafadhali usisite kututumia picha au habari za matukio ya eneo unalo ishi kupitia ukurasa wetu wa ‘Mawasiliano’ au Anuani zetu pepe hapo chini, ili tuzifikishe kwa Watanzania wenzio. Ni matumaini yetu kuwa lugha za kiungwana zitatumika wakati wote wa utoaji maoni katika mtandao huu, kwani lugha za matusi, vitisho na kejeli hazito vumilika.

Asanteni sana kwa ushirikiano wenu.

Timu ya TheHabari

mushi@dev.kisakuzi.com

rungwe@dev.kisakuzi.com

muze@dev.kisakuzi.com

Google+