Guardiola Atimuliwa Barcelona

hi-res-b2df584e0b51a1e54b0923057726ef0a_crop_north
Mshambuliaji Sergi Guardiola alikuwa amesaini mkataba wa kujiunga na timu ya akiba ya Barcelona, lanini ndoto zake zimeota mbawa ya kuchezea timu hiyo

Saa chache baada ya Kusaini, maafisa wa klabu walijulishwa kuhusu jumbe za kuudhi kwenye Twitter” ambazo aliziandika miaka miwili iliyopita kuhusu Barca na jimbo la Catalona.
sergi-guardiola-signs-for-barcelona-dec-2015
Guardiola, 24, aijiunga na Barcelona B Jumatatu, lakini kwa mujibu wa gazeti la michezo la Uhispania la Marca, mkataba wake ulibatilishwa baada ya klabu kugundua alikuwa ameandika jumbe za kuunga mkono mahasimu wakuu wa Barcelona Real Madrid kwenye Twitter.

Aidha, alikuwa ametumia lugha ya kuudhi dhidi ya wakazi wa Catalona, jimbo linalopigania kujitenga kutoka kwa Uhispania.
Guardiola alianza msimu huu akichezea klabu ya Alcorcon ya jiji la Madrid ambayo imekuwa ikicheza ligi ya daraja la pili Uhispania.