Picha juu na chini ni Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira. Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro imeamua kuialika kampuni ya usafi ya Green Waste Pro baada ya kuona juhudi zao za kuweka Manispaa ya Ilala safi na mabadiliko yanaonekana ndipo wakaamua kushirikiana nao katika zoezi la kusafisha fukwe hizo.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency wakishirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro kusafisha fukwe za Kivukoni Front jijini Dar zilizopo mbele ya hoteli hiyo ikiwa ni utaratibu wa hoteli hiyo iliyojipangia kufanya zoezi hilo mara moja kwa mwezi ili kutunza mazingira.
Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) akishiriki zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Kivukoni Front baada ya kupata mwaliko kutoka Hoteli ya Hyatt Regency wa kushiriki katika kusafisha fukwe hizo.
Mwananchi asiyefahamika akiwa amechapa usingizi huku akiwa amejifunika gunia chafu na kulifanya kuwa shuka katika kichaka cha fukwe za Kivukoni Front wakati zoezi la usafi likiendelea. WADAU huyu jamaa hatuna uhakika kama naye ni sehemu ya uchafu au ndio nyumbani?? Tembea uone.
Picha juu na chini ni Baadhi ya Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro wakiwa wamebeba mafurushi ya lundo la uchafu uliokusanywa kutoka kwenye fukwe za Kivukoni Front zilizopo karibu na Hoteli hiyo.
Moja ya magari ya kukusanya uchafu ya kampuni ya Green Waste Pro likiwa limesheheni lundo la uchafu uliokusanywa toka kwenye Fukwe za Kivukoni Front baada ya kusafishwa na Hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro kwa kushirikiana na kampuni ya usafi ya Green Waste Pro.
Wafanyakazi wa Hoteli ya Hyatt Regency na wafanyakazi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro ltd wakibadilishana mawazo baada ya kuhitimisha zoezi la kusafisha fukwe za Kivukoni Front na kuishukuru kampuni ya Green Waste Pro kwa kuitikia wito.
Picha ya pamoja ya Wafanyakazi wa Hyatt Regency na kampuni ya Green Waste Pro baada ya zoezi la usafi.