Mo Blog: Wewe ni mbunifu mwenye jina kubwa hapa nchini na nje ya nchi hii ulianza lini?
Grabriel Mollel: Mimi naitwa Grabriel Molle ni mbunifu wa mavazi ninamiliki Kampuni inaitwa Sairiamu Design ambayo nimeanzisha kutoka mwaka 2009.
Mo Blog: Nini mafanikio yako tangu uingie kwenye fani hii ya ubinifu.?
Grabriel Mollel: Unajua mafanikio sio kuwa na hela benki ila unaangalia umetoka wapi na uliowakuta wamefanya nini na wewe umefika wapi..! Kwa sababu ni mwaka 2010 tu nilifanikiwa kuingia katika Maonesho ya Swahili Fashion ambayo kwangu nahesabu kama ni moja ya mafanikio yangu.
Mwaka 2011 nilifanikiwa kwenda Angola ambapo Swahili Fashion walinichagua tukiwa na Mustafa Hassanali, lakini vile vile Millen Magesse alitufanya sisi tukawa wageni maalum katika onesho la African Fashion Week la Afrika Kusini ambapo hapo nilijifunza mambo mengi sana.
2012 mwezi wa tatu nilifanikiwa kwenda Kampala ambapo mimi mwenyewe ndio nilikuwa ‘Main Designer’, kwa sababu ma-designer wengine walionyesha nguo 10 lakini mimi nilionyesha nguo 25, ikiwemo nguo moja wa ‘Ufukweni’ (Beach wear) ambapo kwa namna nilivyoibuni hapa Tanzania huwezi kuonyesha lakini Uganda unaweza ndio maana nikaenda kufanya ‘launch’ kule Kampala.
Pia sasa hivi nina ofisi tatu, mbili ziko eneo la Makumbusho, moja wapo ikiwa ni ofisi yangu binafsi, na nyingine inahusika na uzalishaji na bidhaa zangu wako watu ambao wanatembeza jioni na pia nina wateja wa nje.
Tangu 2003 nimekuwa nikimiliki ofisi ambayo iko Slipway japo ni gharama lakini siku zote ukitaka kupata fedha inabidi utumie fedha. Lakini ofisi yangu kwa pale inajulikana kama Masai Art Shop lakini iko chini ya Brand ya Sairiamu Designs.
Bofya hapa Kusoma mahojiano yote.