Yule Gavana aliyejiudhuru kutoka jimbo la Illinois hapa Marekani, Rod Blagojevich amepatikana na hatia huko Chicago katika kesi ya rushwa iliyokuwa inamkabili. Mkuu huyo anayefahamika zaidi kwa ile kashfa ya kutaka “kuuza” nafasi ya Ubunge wa jimbo la Illinois, iliyoachwa wazi na Rais Obama baada ya kuchaguliwa kuwa rais mwaka 2008.
Mbali na kesi ya kuuza kiti cha Obama, Blagojevich anakabiliwa na kesi mbalimbali za rushwa, ambazo baada ya hukumu hii anayo hatari ya kwenda jela mpaka miaka 300 kwa mujibu wa mazingira ya makosa aliyotenda. Pamoja na hayo, wachunguzi wa sheria za Marekani wanadai kuwa anaweza akaswekwa ndani kati ya miaka sita hadi 12 tu.
Hii ni mara ya pili kwa jimbo la Illinois kumtuhumu mkuu wa jimbo kwa rushwa, na hatimaye kumtia hatiani. Mkuu wa jimbo hilo kabla ya Blagojevich, George Ryan sasa hivi anatumikia miaka 6 na nusu gerezani.
Source: Yahoo News
Tafsiri: dev.kisakuzi.com