TEKNOLOJIA waliyotumia Google kutengeneza miwani ambayo ina uwezo wa kumpiga picha mtu au kurekodi bila muhusika kujua (google glass) sio mpya ila Kampuni ya Google ndio wakwanza kuja na teknoloji hiyo, ili kila mtu aweze kutumia na inakadiriwa huwenda bidhaa hii ikafanya vizuri sana katika mauzo.
Google glass ni rahisi sana kutumia, kama unataka kupiga picha unachotakiwa kusema ni “OK Glass, take a picture.” upo kwenye foleni unaona fujo unataka kuchukua video, mwambie Google Glass naye atakusaidia kuchukua video. Hii ndio kali, unataka kuwaonyesha ndugu na marafiki kitu unachokiona wakati huo huo? Google glass inafanya yote hayo, inakuja na kitu kama “Skype-style video chat”.
Umesafiri kwenda kuchukua mzigo China? Google glass itakusaidia kuchukua kutafsiri lugha. Umeenda Zanzibar kutembelea majengo ya kitalii na unabaki kushangaa shangaa, uliza Google glass na itakupa tour guide.
Google glass ni kifaa ambacho unaweza kutumia kurekodi video, kupiga picha, kutafuta habari katika Google, kutafsiri lugha, na unaweza fanya yote haya bila kutumia mikoni yako (hands free). Tatizo ni kwamba, ukishavaa hiki kifaa kama miwani, watu hawajui kama unawarekodi kwenye video au vipi, na kwa wabongo walivyo wanavyojua kujihami kupigwa picha au kurekodiwa kwenye video, ukivaa Google glass unaweza tolewa baa.
Kwa nchini Tanzania kifaa hiki ambacho kitakuwa na wastani wa bei ya sh. mil 2. 2 ($1500). Hata hivyo kifaa hicho kinachovaliwa kama miwani, sijui kama utaweza kutembea nacho hata hatua kumi kabla ya vibaka kukuvaa baada ya kujua thamani yake. Tusubiri Google wakiwezeshe kifaa hiki kiweze elewa kiswahili ndio na sisi tutakifaidi zaidi kwani hapa hamna kubonyeza bonyesha ni kuongea tu. Je ukipata Google glass utatumia kifaa hiki cha kisasa kufanyia nini? Acha maoni yako.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com