GOLKIPA wa timu ya taifa ya Uholanzi ameipeleka timu yake katika hatua ya Nusu Fainali za Michezo ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya kupangua penati mbili za wachezaji wa Costa Rica kwenye mikwaju ya penati.
Timu zote mbili zililazimika kwenda kwenye mikwaju ya penati kupata mshindi baada ya kucheza kwa dakika 120 bila kufungana. Costa Rika ambao muda mwingi walicheza kwa kuzuia zaidi ya kushambulia walijikuta wakitolewa kwenye mikwaju ya penati baada ya kufungwa magoli 4-3.
Shujaa katika mchezo huo aliibuka golkipa wa Uholanzi baada ya kuingia dakika ya 120 ya mchezo kwa kazi maalumu tu ya kudaka mikwaju ya penati, alijikuta akifanikiwa zaidi pale alipopangua mikwaju miwili ya wachezaji wa Costa Rica hivyo kuiingiza timu yake katika hatua ya nusu fainali za mashindano hayo.
Wachezaji wa Uholazi walionekana makini zaidi katika upigaji wa mikwaju ya penati ambapo hakuna aliyekosa kati ya penati 4 walizopiga. hivyo hadi mwisho wa mchezo Uholanzi 4 na Costa Rica 3. Katika mchezo wa awali kati ya timu za Argentina na Belgium ulimalizika kwa timu ya Argetina kuibuka kidedea baada ya kupata goli moja la pekee katika dakika ya nane ya mchezo huo. Hivyo hadi mwisho wa dakika 90 za mchezo huo Argentina 1 na Belgium sifuri.