Godauni la Magurudumu Lawaka Moto Sinza Lego, Dar

Moto ukiwaka jioni hii kwenye godauni moja lililopo eneo la Sinza Lego, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa kijana ambaye alifika kushuhudia tukio hilo akijaribu kupanda juu ya ghorofa baada ya kunusurika kudondokea katika moto huo.

Moto ukiendelea kuwaka huku juhudi za kuzima zikiendelea

 

Moto ukiendelea kuwaka katika godauni hilo.
Baadhi ya wananchi wakishuhudia tukio hilo la kuwaka kwa godauni.
Magari yakiwa yameruhusiwa kuendelea na safari baada ya moto huo na moshi mkubwa kupungua.

Godauni moja lililopo maeneo maeneo ya Sinza Lego, ambalo lilikuwa la kuhifadhia magurudumu ya gari pamoja na vifaa vyingine vya magari ambalo mmiliki wake hakuweza kufahamika mara moja limeteketea kwa moto. Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo kimetokana na magurudumu kushika moto. 
Hadi majira ya jioni kikosi cha kuzima moto kilikuwa eneo la tukio kuendelea kusaidiana na wananchi kuuzima moto huo. Haikiweza kubainika athari za moto huo kwa mara moja. Taarifa kamili itatolewa na Jeshi la Polisi.
Chanzo; Blogs za Mikoa