Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam, kuhusu kongamano kubwa la vijana litakalofanyika Zanzibar kwa kipindi cha mwezi mzima kuanzia Julai 12 mwaka huu. Kongamano hilo litahudhuriwa na marais wastafu na viongozi maarufu. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi na Mratibu wa kongamano hilo, Antu Mandosa
Mwakilishi Mkazi wa GPF nchini, Martha Nghambi (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kulia ni Balozi wa Amani, Risasi Mwaulanga na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Global Peace Foundation (GPF), Arnold Kashembe.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
SHIRIKA la Global Peace Foundation limewataka Watanzania kudumisha amani iliyopo ili nchi yetu isije ikakumbwa na machafuko kama nchi za jirani.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Global Peace Foundation na Mshauri wa Amani Afrika , Arnold Kashembe alisema Shirika hilo limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC).
“Shirika la GPF limeandaa mkutano wa kujadili mkakati wa kudumisha amani utakao jumuisha nchi za Afrika Mashariki (EAC) ambao utafanyika Zanzibar kuanzia Julai 21- 24,” alisema Kashembe.
Kashembe alisema mkutano huo wa kipekee utawakutanisha maraisi wastaafu nane akiwemo Keneth Kaunda na Amani Karume, viongozi wa dini, wafanyabiashara na viongozi wengine kutoka nchi za Afrika Mashariki na nchi jirani.
Aidha Global Peace Leadership Conference (GPLC) 2015 itatoa mafunzo na nyenzo ili kuhimiza ushirikiano katika ukanda wa Afrika Mashariki na kujaribu kupunguza tofauti na matatizo yanayowakumba.
Mada nyingine ni kuwapongeza vijana 400 kutoka Afrika Mashariki wanaotarajiwa kushiriki kuongeza nguvu katika mbinu za ujasiriamali na kuwa mfano wa wanafunzi wa wengine huko watokapo.
Kujenga mikakati imara ya kudumisha ukaribu na kusaidiana mbinu za kupambana na umaskini, tatizo la ajira, HIV, Malaria na kuwezesha na kuzindua misheni Maendeleo ya Afrika kama lengo kuu na kiini cha mabadiliko kupitia Amani, Uongozi bora, na Uimara wa maendeleo kiuchumi.