GLAUCOMA: Mwizi wa Macho ya Watu Kimyakimya

Hospitali ya Apollo ambayo inayohudumia watoto zaidi.

Hospitali ya Apollo ambayo inayohudumia watoto zaidi.


MWEZI Januari kila mwaka Jumuiya za Kimataifa uungana ili kuongeza uelewa na kujenga ufahamu juu ya ugonjwa wa Glaucoma. Kampeni hii ya mwezi mzima inalenga kuleta tahadhari na kuelimisha juu ya chanzo, sababu na madhara ya ugonjwa huo, kampeni hii pia ulenga kuutaka umma kuchukua hatua madhubuti kabla ugonjwa huu mbaya haujasababisha athari kubwa.
Kutokana na asili ya ugonjwa huu imesababisha ujulikane kama “the sneak thief of sight”, yaani mwizi wa macho anayekuja kwa kunyata. Hii inatokana na kuwa ugonjwa huu mbaya hauna dalili, unakuja taratibu sana na ghafla mtu hupoteza uwezo wa kuona na kupata upofu wa kudumu.
Ugonjwa wa Glaucoma unaripotiwa kuwa moja ya sababu zinazoongoza katika kusababisha upofu duniani. Shirika la Afya Duniani (WHO) linakadiria kuwa watu milioni 4.5 duniani kote ni vipofu kutokana na ugonjwa huo. Shirika la utafiti wa Glaucoma (GRF) linasema kwamba “zaidi ya 40% ya uwezo wa kuona inaweza kupotea bila mtu bila mtu kujua”.
Tanzania kama nchi nyingine nyingi duniani kote ni mwathirika wa ugonjwa huu wa macho. Hata hivyo ukubwa halisi wa madhara kwa umma kwa ujumla bado haujulikani katika jamii kutokana na kiwango cha chini cha ufahamu ambao upo sasa.
Habari ya kutosha, elimu na mkakati wa mawasiliano inahitajika kuundwa ili kuongeza uelewa na maarifa ya jamii ya Tanzania kuhusu ugonjwa ili kuwezesha utambuzi wa mapema na matibabu wakati muafaka kwa waathirika wa hali hii.
Kulingana na ripoti ya Idara ya macho ya hosipital ya KCMC iliyochapishwa tarehe 30 Septemba 2014, katika mwaka 2012 peke yake watu 328,535 wenye umri wa miaka 40 na zaidi waligundulika kuwa na ugonjwa huu nchini Tanzania. Takwimu hii haijumuishi ya wangonjwa waliozaliwa nao, vijana na watoto.
Kama moja ya mkakati wa kupambana na ugonjwa huu nchini Tanzania, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii imeunda mpango mkakati wa Taifa wa huduma ya macho. Ambapo kupitia huo huduma za macho zitaboreshwa nchi nzima.

“Uboreshaji huo unaotarajiwa kufanyika chini ya mpango mkakati kuanzia 2011-2016 utachangia kufanikisha utekelezaji wa Global Vision 2020,”. Amebaini Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk Seif Rashid.

Dk Binita Thakore, Mtaalam na Mshauri wa magonjwa ya macho na Glaucoma Mtaalamu katika hospital ya Apollo, anadai kwamba, Glaucoma ni ugonjwa wa pili unaoongoza kwa kusababisha upofu duniani kote. Katika kila watu 100, zaidi ya 4.5 wana aina hii ya ugonjwa.

Glaucoma si jina la ugonjwa wa jicho peke, bali inahusu kundi la magonjwa ya macho ambayo inakusababishia upofu taratibu siku had siku bila dalili yoyote. Upofu huo unasababishwa na kuharibika kwa neva ya macho. Neva hii ipo kama kebo ya umeme wenye nyaya zaidi ya million na ndio inakazi ya kupeleka taswira kwenye ubongo. Shinikizo kwenye jicho ndio chanzo cha uharibifu wa neva za macho.
Glaucoma inasababishwa na maji maji yanayoingia na kutoka kwenye jicho. Majimaji hayo sio machozi na yanapatikana juu ya uso wa nje wa jicho. Dk Thakore anasema, “Unaweza kupata picha ya mtiririko wa maji kwenye bomba lililopo kwenye sinki na limefunguliwa wakati wote. Sinki hiyo ikizibwa maji hujikusanya na kusababisha presha ndivyo ilivo katika macho pia presha ikiongezeka inaweza kuharibu neva za macho. Endapo neva za macho zikiharibiwa, mtu hupoteza uwezo wa kuona na kamwe hawezi kupona.
Kuna aina mbalimbali za Glaucoma, ikiwa ni pamoja na primary open angle glaucoma ambayo ni glaucoma kawaida duniani kote. Mirija ya maji pembeni ya macho inachoka kadri muda unavoenda, na shinikizo ndani ya macho hatua kwa hatua kuongezeka. Aina ya pili ni primary angle closure glaucoma aina hii ya ugonjwa inafahamika sana.
Hapa mirija inakosa uwezo wa kutoa majimaji nje ya jicho na hivyo kusababisha presha ndani ya jicho. Aina nyingine ni ile ya kuzaliwa. Hii hutokea mara 1 katika watoto 1,000 wanaozaliwa na inaweza kusababisha upofu takriban 10% ya kesi.
Glaucoma ya kuzaliwa nayo inatokana na matatizo ya mfumo. Kutokana kwamba macho ya watoto wachanga yanaongezeka, yanaongezeka na yanakuwa na rangi nyeupe. Vitu kama majeruhi kwa jicho, baadhi ya dawa na magonjwa ambayo yanaweza kuzuia kutoka kwa majimaji yana changia kusababisha glaucoma. Wagonjwa wa pumu, mzio wa ngozi na magonjwa ya macho mara nyingi hutumia, madawa, kirimu au dawa za macho zenye steroidi ambayo inaweza kusababisha glaucoma.
Kuhitimisha juu ya athari za ugonjwa wa glaucoma Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Hospitali za Apollo Dr. Prathap C. Reddy anasema kwamba “ugonjwa wa glaucoma unaweza kuiba uwezo wa kuona kimya kimya kiasi kwamba mgonjwa anaweza kuwa hajui mpaka pale neva za macho zitakapokuwa zimeharibiwa vibaya. Kwa sababu hakuna dalili zozote za mwanzo, njia bora ni kutambua ugonjwa huu kupitia uchunguzi mara kwa mara ya matibabu ya macho. Mara nyingi glaucoma haiwezi kutibiwa. Matibabu hutolewa ili kuhifadhi uwezo mdogo wa kuona uliobakia. Anaongeza kuwa “Ni vizuri kufanya uchunguzi wa kina wa glaucoma kabla ya mpango wowote wa matibabu”.
Mwenyekiti wa Apollo anatoa wito kwa ajili ya uchunguzi wa macho mara kwa mara ni utamaduni ambao Watanzania wanatakiwa kujijengea. Kwani tofauti na maradhi mengine mengi, glaucoma ina uwezo wa kusababisha upofu na mgonjwa asiweze kupatiwa matibabu tena.