Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika matembezi ya Maadhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania (TGGA) ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho Duniami, Roden Barden Powell yaliyofanyika Manispaa ya Temeke Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TGGA Tanzania, Profesa Martha Qorro na Kamishna Mkuu wa TGGA Tanzania, Symphorosa Hangi.
Wanafunzi wanachama wa TGGA Temeke wakiandamana wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Shule ya Tandika wilayani Temeke, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Viongozi wa TGGA wakipiga makofi wakati wa kuyapokea matembezi ya wanachama wa TGGA.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA.
Kaimu Ofisa Tarafa Chang’ombe, Hezron Mweladzi (kushoto) aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva akizungumza jambo wakati wa Madhimisho ya Chama Cha Girl Guides Tanzania ya kumuenzi mwanzilishi wa chama hicho. Roden Barden Powell… Kulia ni Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi na Mwenyekiti wa Chama hicho,Martha Qorro.
Wanafunzi hao wakiimba nyimbo wakati wa maadhimisho hayo.
Wanafunzi wakiwa katika igizo la mchezo wa kuelimisha na kukataa kurubuniwa na wanaume. wa katikati ni Eunice Joseph, kushoto ni Hajra Mhamedy na kulia ni Seiph Kingwande.
Wanafunzi wakiwa katika igizo, kushoto ni Eunice Joseph kama mwanafunzi, kulia aliyekaachini ni ni kama Daktari aliyekuwa akimpima mwanafunzi aliyekuwa na ujauzito Husna Mussa na wakatikati ni Farider Mohammed kama mzazi wa mwanafunzi.
Kamishna wa TGGA Temeke, Komba akizungumza jambo wakati wa maadhimisho hayo.
Profesa Qorro akihutubia wakati wa maadhimisho hayo.
Profesa Qorro akiwaelekeza jambo wanafunzi.
Profesa Qorro akiagana na wanafunzi baada ya maadhimisho hayo kumalizika.