Ghana Yaibuka Mshindi wa Nusu Fainali Guinness Football Challenge

Naab Jonathan Baan na Desmonf Odaano wa Ghana katika picha na watangazaji wa kipindi hicho

Francis Wangari na Kepha Kimani wa Kenya

JANA usiku (Mei 22 2013) kupitia televisheni za ITV na Clouds TV nusu fainali ya kwanza kabisa ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™ ilirushwa hewani na katika runinga Afrika nzima ambapo timu ya Ghana ilionesha ni kwanini ni timu bora ambayo ndiyo imejishindia pesa nyingi mpaka sasa.

Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha uwezo na ujasiri wao walipoibuka washindi zidi ya wapinzani wao timu kutoka Kenya katika mchezo wa jana. Katika hatua ya pesa ukutani walifanikiwa kulenga lango namba nne na hivyo kupata dola za kimarekani 12,000 wanazoziongeza katika dola 8,500 walizokuwa nazo awali katika hatua ya robo fainali.

Wakenya Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao ni washindi wa pili katika nusu fainali hii wataungana na Ghana katika fainali.Ingawa waliikosakosa hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness bado wana nafasi ya kuwa mabingwa katika fainali.

Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™. Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.

Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania

Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.