Geofrey Mungai Awasaidia Yatima wa Daily Bread Life

Geofrey na mkewe  wakiwaongoza  watoto yatima  kupata chakula.

Geofrey na mkewe wakiwaongoza watoto yatima kupata chakula.

Bi  Sarah Mungai akiwa na mmoja kati ya  watoto yatima wa kituo cha DBL mkimbizi Iringa
Bi  sarah Mungai akiwa na Mtoto  aliyetupwa na  mama  yake  mzazi ambae anautindia  wa  ubongo  mara  baada ya  kumzaa na sasa anaendelea vema baada ya  kuokolewa maisha yake  na kituo cha DBL Iringa
Mkurugenzi wa kituo  cha DBL Neema Mpeli  kulia akiwa na sarah Mungai
Mkurugenzi Mtendaji wa DBL Mchungaji Mpeli Mwaisumbi akimkaribisha  Mungai na mkewe
Baadhi ya  watoto  kituoni hapo
Mchungaji Mpeli  akieleza jinsi ambavyo Mungai alivyokuwa msaada  kituoni hapo

MKANDARASI Geofrey Mungai ametoa msaada wa nguo za sikukuu na chakula vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Tsh milioni 2 wa kituo cha watoto yatima cha Daily Bread Life Tanzania (DBL) kwa ajili ya kusherekea siku kuu ya Krismass na mwaka mpya. Mungai alitoa msaada huo jana kwa uongozi wa kituo hicho pamoja na kuwaandalia chakula cha pamoja watoto zaidi 39 na wananchi mbalimbali wa mji wa Iringa kama njia ya kuwahamasisha kusaidia yatima.Akizungumza kwa niaba ya familia ya Mungai mke wa mkandarasi huyo Sarah Mungai alisema kuwa imekuwa ni kawaida yake kwa kila mwaka katika msimu wa sikukuu ya Krismas na mwaka mpya kufika katika kituo hicho na kuwapa msaada watoto hao ili nao kuungana na watoto wenye wazazi wao kufurahia sikukuu hizo.Hata hivyo alisema kuwa jamii ya Mkoa wa Iringa na watanzania kwa ujumla wanapaswa kubadilika kwa kuelekeza michango yao kwa watoto yatima ambao baada ya kupoteza wazazi wao faraja ya pekee  wanaisubiri kutoka kwa jamii inayowazunguka.Aidha alisema kuwa yeye kama mmoja kati ya wananchi wa Iringa wenye mapenzi mema na watoto yatima hivyo kuwaomba wananchi wengine kuweka mpango wa kuendelea kutembelea vituo vya yatima kila mwaka kwa ajili ya kuwasaidia misaada mbalimbali.Alisema kuwa upo uwezekano mkubwa wa watoto hao yatima kuendelea kusaidia iwapo watanzania na wadau mbalimbali kuwekeza kwa watoto hao. Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Mchungaji Mpeli Mwaisumbi mbali ya kumpongeza Mungai kwa kuendelea kusaidia watoto hao bado wadau mbalimbali wameendelea kujitolea kusaidia kituo hicho. “Watoto hao wanalilewa vema na wapo ambao wanasoma shule mbalimbali na vyuo vikuu baada ya usaidiwa na wadau”Alisema kuwa kituo hicho kinafanya kazi chini ya shirika lisilo la kiserikali ya Daily Bread Life Tanzania lililosajiliwa kwa usajili 12903 chini ya wizara ya mambo ya ndani ya nchi pia kituo  kimesajiliwa na ustawi wa jamii kwa kupewa usajili wa makao ya watoto namba 00049995.Hata hivyo alisema kuwa kituo kilianza kupokea watoto 14 mwaka 2004 na sasa kuna watoto 37 waliopo kituoni hapo na kuwa toka kituo kianzishwe jumla ya watoto 51 wamelelewa hapo. Alisema kutokana na misaada wa wadau mbalimbali kituo kimeendelea kupata mafanikio makubwa kama kuwa na shamba, basi moja, mradi wa cherehani pia tayari shule ya sekondari ya DBL imejengwa na imeanza kupokea wanafunzi toka mwaka huu shule iliyopo umbali wa kilomita 6 kutoka mjini Iringa kwa lengo kuwawezesha watoto na wengine watyakaofaulu na kukosa nafasi kupata elimu ya sekondari.Pia alisema changamoto kubwa katika uendeshaji wa kituo hicho ni michango mingi katika shule za msingi ambako watoto hao wanasoma, kukosa ruzuku toka serikalini na changamoto nyingine nyingi. Mchungaji Mpeli aliwaomba watanzania na wadau mbalimbali pale walipo iwapo wanahitaji kusaidia kituo hicho kutuma michango yao kupitia akaunti namba Benk ya Exim ni 5435526007 Daily Bread Life Childreans home, ama kwa njia ya M-PESA 0754362536.