Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United na Timu ya taifa ya Uingereza Gary Neville ametangazwa kuwa Kocha mpya wa Klabu ya Valencia.
Jina la Neville limewashitua wengi mara baada ya kutangazwa hapo jana kuwa Meneja Mpya wa kikosi hicho kinacho shiriki ligi kuu ya Uhispania hadi mwishoni mwa Msimu.
Kibarua cha kwanza kwa Gwiji huyo kitakuwa katika mchezo wa ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya timu ya Lyon hapo Disemba 9.
Akizungumza na mtandanao wa Klabu hiyo Neville alikiri kuwa na kiu ya kupata nafasi kama hiyo kwa muda mrefu ndani ya klabu ya Valencia.
“Klabu ya Valencia ni moja ya Klabu kubwa Dunian, tangu nikiwa mchezaji nilikuwa kipenzi kikubwa cha Valencia hivyo kufanya kazi nao naona nimekamilisha ndoto yangu ya muda mrefu”.
“Najua kuna changamoto nyingi, ila ninachoangalia kwa sasa ni kuhakikisha tunakuwa na mafanikio pamoja na wachezaji nilionao”
Naye Raisi wa Valencia Layhoon Chan, aliongeza kuwa “tumeamua kuchukua maamuzi ya haraka kwa Gary kwa sababu ni Kocha mwenye uzoefu Mkubwa tangu akiwa mchezaji wa Manchester na kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Uingereza hivyo tunaona anatufaa.”
Neville anachukua mikoba ya Nuno Espirito Santo, ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alipoteza mchezo wake dhidi ya sevilla kwa kuchapwa Bao 1-0.