Tunawashukuru wadau wote wa Mtandao wa WWW.FULLSHAANGWEBLOG.COM kwa uvumilivu wenu baada ya mtandao wetu kutokuwa hewani kwa siku mbili kutokana na matatizo yaliyokuwa nje ya uwezo wetu. Tunapenda kuwaarifu kuwa mtandao wa FULLSHANGWEBLOG umerejea usiku wa kuamkia leo mara baada timu ya wataalam wetu kukamilisha kazi ya marekebisho na tayari tumeanza usiku huo huo.
Tunashukuru kwa uvumilivu wenu na kutuelewa kila mlipotupigia simu kuulizia hali ikoje, tunawashukuru pia kwa simu zenu kwani tumejiona ni wenye bahati na mchango wetu mnautambua vizuri.
Tunatoa shukurani kwa wadau wetu wawezeshaji Benki ya NBC, Benki ya NMB, NHIF, TTB, SERENGETI BREWERIERS, WILNA INTERNATIONAL, BAYPORT na R&R kwa uvumulivu wenu. Tunasema asanteni sana na Mablogger wote ambao walitusemea wakati tulipokuwa na tatizo hili.
Shukurani za Pekee zimwendee Mustafa Selemani mtaalam wetu na timu yake kwa kuhakikisha wanarekebisha tatizo hilo mpaka tunarejea tena hewani usiku wa kuamkia leo, tunamshukuru Mustafa pamoja na timu yake ya G5CLICK.
Mwisho tunasema kazi inaendelea mbele na wadau wote mnakaribishwa kututumia habari na matukio mbalimbali kupitia barua pepe johnbukuku@gmail.com au info@fullshangweblog.com.