Fujo za Mashabiki wa Diamond Zasababisha Hasara ya Mil. 600

Baadhi ya Polisi wa Ujerumani wakiwa wamelizunguka gari alilopanda Diamond kumnusuru na hasira za mashabiki.

Baadhi ya Polisi wa Ujerumani wakiwa wamelizunguka gari alilopanda Diamond kumnusuru na hasira za mashabiki.

Msanii Diamond akiondolewa chupu chupu katika mikono ya wenye hasira

Msanii Diamond akiondolewa chupu chupu katika mikono ya wenye hasira

Muonekano wa jukwaa mbele na meza zilizoitwa VIP zilizolipiwa euro 100 kwa wahusika, kiingilio cha kawaida kilikuwa euro 25.

Muonekano wa jukwaa mbele na meza zilizoitwa VIP zilizolipiwa euro 100 kwa wahusika, kiingilio cha kawaida kilikuwa euro 25.

Muonekano wa ukumbi baada ya vurugu kufanyika.

Muonekano wa ukumbi baada ya vurugu kufanyika.

*Promota wa onesho hilo, Awin Williams Matatani

FUJO zilizofanywa nchini Ujerumani na mashabiki na wapenzi wa msanii nyota wa muziki wa bongo fleva kutoka Tanzania, Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz baada ya yeye kuchelewa kuingia ukumbini imegudulika zimesababisha hasara ya Euro 300,000 ikiwa ni takribani shilingi milioni 600 za Kitanzania.

Hasara hiyo imetokana na baadhi ya mashabiki kufanya fujo Agosti 30, 2014 mjini Stuttgart, Ujerumani na kuharibu mali mbalimbali za ukumbi pamoja na vifaa vingine vya muziki vilivyoandaliwa kwa ajili ya onesho hilo, lililovunjika baada ya fujo na mashabiki kutaka kumtwanga Diamond wakilalamikia kitendo cha msanii huyo kuchelewa kwenye onesho hilo takribani zaidi ya masaa matano tofauti na walivyoelekezwa.

Hata hivyo taarifa za polisi wa Ujerumani zimezidi kumtia matatani promota wa onesho hilo, Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria ambaye atalazimika kulipa hasara yote iliyosababishwa na vurugu hizo. Taarifa za awali za polisi wa nchi hiyo wamebainisha kuwa promota huyo alitoa taarifa za uongo wakati akikodisha ukumbi huo na hakuwa na bima ya kulinda mali na hasara ambayo zingeweza kutokea katika onesho.

Taarifa zaidi kutoka kwa baadhi ya wakazi wa mji wa Stuttgart zinasema promota Williams Akpomiemie aliuarifu uongozi wa Ukumbi huo kuwa ilikuwa ikifanyika hafla ya Waafrika pamoja na mkutano lakini sio onesho la muziki kama ilivyofanyika baadae jambo ambalo inadaiwa alitoa taarifa za uongo.

Tayari polisi wa mji huo wamelipeleka suala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt) ya Mji wa Stuttgart kwa hatua zaidi za kisheria hatua ambayo inamweka roho juu zaidi promota Awin Williams Akpomiemie wa kampuni ya Britts.

Wakati huo huo taasisi mbalimbali na Jumuiya za Waafrika nchini Ujerumani zimelaani vikali tukio hilo pamoja na hasara iliyojitokeza na kudai matukio kama hayo yanalichafua bara la Afrika hivyo kuwataka watu wajiepushe na tabia kama hizo.

Zaidi:- http://www.modernghana.com/news/567209/1/african-diaspora-is-still-bleeding-diamonds-nightm.html