Friends Rangers Kuivaa Majimaji ya Songea Dar

Ofisa Habari wa timu ya Friends Rangers, Asha Kigundula.

Ofisa Habari wa timu ya Friends Rangers, Asha Kigundula.

Mwandishi Wetu

KIKOSI cha timu ya Friends Rangers, kesho kinajitupa kwenye Uwanja wa Karume kuvaa na timu ya Majimaji ya Songea, katika mchezo wa Ligi Daraja la kwanza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa timu hiyo Asha Kigundula, alisema kuwa wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka katika timu hiyo ambayo mpaka sasa ndiyo inaongoza ligi, wakati wao wakishika nafasi ya pili.

Kigundula alisema kikosi chao tayari kipo kambini kikijiandaa na mchezo huo, huku kocha wao Ally Yusuph ‘Tigana’ akijipanga kuhakikisha pointi tatu zinabaki nyumbani. Pia Kigundula amewataka wapenzi kujitokeza kwa wingi kuipa ushirikiano timu yao ambayo inapambana kuhakikisha inapanda daraja msimu ujao.

“Kikubwa tukipata ushirikiano kwa wapenzi ambao wamekuwa wakijitokeza kutushangilia mwanzo mwisho naamini tutafanya vizuri…tunaomba mjitokeze kutushangilia tufanye vizuri,” alisema Kigundula.

Rangers ina pointi 16, baada ya kucheza mechi 8 huku wanaoongozawakiwa Majimaji wakitofautiana kwa pointi mbili, endapo Rangers itashinda itakuwa ikiongoza kwa tofauti ya pointi moja. Ikiwa imeshinda mechi nne na kutoka sare mechi nne, huku ikiwa inakimbizana na Majimaji ambayo nayo ina pointi 15.