Flydubai Yatangaza Safari 3 Kuja Tanzania

FlyDubai Boeing 737-800

FlyDubai Boeing 737-800


 
SHIRIKA la ndege lenye makao yake Dubai leo limetangaza uzinduzi wa safari za ndege za Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari za ndege za nchi hii ya Afrika Mashariki zitaanza Oktoba, zikikuza mtandao wa shirika hili la ndege barani Afrika hadi vituo 12.
 
Akizungumzia kuhusu uzinduzi wa safari hizi, Ghaith Al Ghaith, Ofisa Mkuu Mtendaji wa flydubai, alisema: “Kwa kuongeza safari hizi tatu mpya nchini Tanzania tumekuza mtandao wetu mara mbili katika Afrika ya Kaskazini na Mashariki mwaka huu, tukiimarisha ahadi yetu ya kuhudumia masoko ambayo hayakuhudumiwa vya kutosha.”
 
Hivi karibuni flydubai ilitangaza uzinduzi wa safari za ndege za Bunjumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda na safari za vituo hivi zitaanza mwishoni mwa Septemba.
 
Tanzania ni kitovu cha eneo upande wa utalii wa Afrika Mashariki na mwakani 2013 nchi hiyo iliwakaribisha watalii milioni 1. Kulingana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), idadi hii inatarajiwa kuongezeka mara mbili na watalii milioni 2 wakitarajiwa ifikapo 2017.
 
Makamu Mkuu wa Rais wa Biashara, Sudhir Sreedharan (GCC, Bara Dogo na Afrika), alisema, “Mtandao wetu unaoendelea kukua unaunga mkono Dira ya Utalii ya 2020 ya Dubai inayolenga kuwavutia wageni milioni 20 katika Umoja wa Falme za Kiarabu ifikapo 2020.
 
Kwa kutoa huduma za kuaminika, kwa bei nafuu na zilizo rahisi za usafiri kutoka Tanzania, tunawapa abiria fursa ya kusafiri Dubai na kuunganisha safari zao na zaidi ya vituo 200 duniani kote kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai.”
 
Tanzania ni nchi inayojulikana kwa uzuri wake wa asili na wanyamapori. Dar es Salaam ni kitovu cha biashara nchini Tanzania na mji huo una bandari linalovutia na vivutio tele vya kitamaduni na kihistoria. Unguja, inayojulikana kama Kisiwa cha Viungo, imefunikwa na pwani nyeupe na imejaa utamaduni, historia na wanyamapori wanaopatikana huko tu. Zaidi ya hayo, vilele vya Mlima Kilimanjaro vilivyofunikwa na theluji huwakaribisha watalii kwa matembezi na kuteleza juu ya theluji mwaka mzima.
 
flydubai imeunda mtandao mpana barani Afrika ulio na safari za ndege za Addis Ababa nchini Uhabeshi, Alexandria nchini Misri, Khartoum na Port Sudan nchini Sudani, Djibouti mji mkuu wa Djibouti, Juba nchini Sudani Kusini pamoja na Bujumbura nchini Burundi, Entebbe nchini Uganda na Kigali nchini Rwanda.
 
Maelezo ya Safari za Ndege” Dar es Salaam
flydubai itaendesha safari za ndege kila siku kati ya Dubai na Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 Oktoba 2014.
FZ670 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 6:20 machana saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:55 jioni saa za ndani.
FZ672/674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 12:20 jioni saa za ndani, itue katika Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani.
FZ669/671/673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa 5:20 asubuhi saa za ndani.
 
Nauli za safari ya pande zote
Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Dar es Salaam hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1,499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.
 
Kilimanjaro kupitia Dar Es Salaam
flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Kilimanjaro na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 17 Oktoba 2014.
 
Jumatatu na Ijumaa:
FZ674 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 10:10 jioni saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.
 
FZ673 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro saa 7:25 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.
 
Nauliza pande zote mbili
Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Kilimanjaro hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.
 
Zanzibar kupitia Dar Es Salaam
flydubai itaendesha safari mbili za ndege kila wiki kati ya Unguja na Dubai kupitia Dar Es Salaam kuanzia tarehe 19 Oktoba 2014.
 
Jumanne na Jumapili: FZ672 imepangiwa kuondoka Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 9:40 mchana saa za ndani, itue Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 7:00 usiku saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.
 
FZ671 imepangiwa kuondoka Kituo cha 2 cha Kimataifa cha Dubai saa 12:40 asubuhi saa za ndani, iwasili Uwanja wa Ndege wa Unguja saa 7:05 mchana saa za ndani na katizo la safari la saa moja mjini Dar es Salaam.
 
Nauli za safari ya pande mbili
Nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Uchumi kutoka Unguja hadi Dubai itaanzia Dola 399 za Marekani ikijumuisha mzigo wa 20kg uliokaguliwa, huku nauli ya kuenda na kurudi ya Kitengo cha Biashara itaanzia Dola 1499 za Marekani na inajumuisha kodi zote na mzigo wa 40kg uliokaguliwa. Hizi ni nauli maalum za uzinduzi za mwezi mmoja.