Fistula inatibika, toa kwa moyo kumuokoa mama na mtoto

Baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBR, Dar es Salaam wakiimba wakati wa uzinduzi wa kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo. Kwa kuchangia kwa njia ya M-PESA tafadhali tuma kwenda namba 200500, na kwa njia ya SMS tuma ujumbe mfupi usemao MOYO kwenda namba 15599.


Ofisa Mkuu wa masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba, akiimba nyimbo mbalimbali na baadhi ya akina mama wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula katika Hospitali ya CCBR, mara baada ya kuzindua Kampeni ya MOYO, hapo juzi inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa huo hapa nchini, Kwa kuchangia kwa njia ya M-PESA tafadhali tuma kwenda namba 200500, na kwa njia ya SMS tuma ujumbe mfupi usemao MOYO kwenda namba 15599.

Na Mwandishi Wetu

THAMANI ya mwana aijuae mzazi, Wote tumezaliwa na hivyo wote ni watoto. Zaidi ya wanawake 3,000 nchini hupatwa na tatizo la Fistula kila mwaka, Hii hutokea wakati wanapojifungua.

Fistula husababishwa na uchungu wa muda mrefu wakati wa kujifungua baada ya mzazi kutopatiwa huduma kwa muda muafaka kutokana na upungufu au kutokuwapo kwa vifaa vya afya. Hatimae mwanamke hupoteza kichanga chake na pia kujikuta katika hali ngumu ya kupoteza udhibiti wa haja kubwa na ndogo na hivyo kumtoka kwa mfululizo.

Vodacom Tanzania kwa kushirikiana na CCBRT mnamo Februari 5, mwaka huu ilizindua kampeni ya umma MOYO inayolenga kuchangisha fedha kiasi cha sh. bilioni moja kugharamia ujenzi wa Hospitali maalumu ya Afya ya Uzazi na Matibabu ya Bila Malipo kwa wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula nchini.

Mkazi wa jijini Mbeya, Stella Nzyemba, alietibiwa ugonjwa wa Fistula, akisimulia jinsi alivyokata tamaa ya maisha baada ya kuugua ugonjwa huo. Kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni ya MOYO inayolenga kuhamasisha jamii kuchangia fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wenye matatizo ya ugonjwa wa huo hapa nchini, Kwa kuchangia kwa njia ya M-PESA tafadhali tuma kwenda namba 200500, na kwa njia ya SMS tuma ujumbe mfupi usemao MOYO kwenda namba 15599.


“Ugonjwa huu unawatesa mama zetu na dada zetu hasa wanaoishi katika mazingira duni, unawakosesha raha/amani unawasababishia unyonge wa maisha na upweke hata kunyanyapaliwa, kukimbiwa na waume ambapo ni miongoni mwa athari kadhaa za kisaikolojia.alisema,” Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Bi. Mwamvita Makamba.

Vodacom tangu mwaka 2010 imekuwa ikisihirikiana na Hospitali ya CCBRT katika program ya kuwapatia fedha wanawake wenye matatizo ya Fistula kugharamia nauli za kutoka sehemu mbalimbali nchini kupitia M-PESA kuwawezesha kufika jijini Dar es salaam kupata matibabu.

Kila mmoja anayo nafasi ya kuonesha upendo na thamani kwa mama kwa kuokoa maisha yao, Taasisi za Umma na Binafsi, mtu binfasi ama shirika la kijamii changia sasa kwa njia ya M-PESA kwenda namba 200500, au na kwa njia ya SMS kwa tuma ujumbe usemao MOYO kwenda namba 15599.
Kama sio wewe basi jirani au rafiki anaweza kuwa shahidi wa jambo hili.