Filamu ya SAYLA kuzinduliwa Arusha

FILAMU ya SAYLA inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Julai 13, 2012 katika Jiji la Arusha. Filamu hiyo iliyoshirikisha wasanii na watu maarufu takribani 27 imeandaliwa maalum kwa ajili ya kuonesha matumizi ya sanaa, kwa Watanzania na namna ya kusaidiana wakati wa matatizo. 

Filamu hii maalum kwa ajili ya kuwasaidia Sajuki na Wastara waliokuwa katika wakati mgumu wa kutafuta pesa za matibabu, itazinduliwa kwenye ukumbi wa Naura Springs na kuhudhuriwa na watu wengi maarufu nchini akiwemo Mh Shyrose Bhanji na wabunge wengine wa  Bunge la Afrika Mashariki, Wema Sepetu akiongoza kundi la wasanii wa Bongo Movie pamoja na wengine kama Snura, Shilole ambao watatumbuiza kwa kushirikiana na Ndege mnana Linah, kwa mara ya kwanza jijini Arusha toka adondoke.

SAYLA ni filamu ya kihistoria iliyoshirikisha idadi ya kubwa ya mastaa kuliko yeyote ile, itazinduliwa pamoja na video na behind the scene za nyimbo ya Mboni yangu!
Baadhi ya watu walioshiriki kwenye hiyo project ni kama ifuatavyo: Mh Zitto Kabwe, Mh January Makamba, Mh Halima Mdee, Mh Esther Bulaya, Mh Vicky Kamata, Mh Shyrose Bhanji, Mzee Chillo, Mzee Hashim Kambi, Muhogo Mchungu, Bi Kidude, Sharo Milionea, Mboto, Kitale, Wema Sepetu, Davina, Ephrahim Kibonde, Adam Mchomvu, Arnold Kayanda, George Goyayi, Mairmatha wa Jesse, Rose Chitala, Ruben Ndege, Irene Paul, Dully Sykes, Chege, Madee, Recho, Ommy Dimples, William Mtitu, Mwana FA na wengine wengi.
Filamu hiyo imetayarishwa na timu kubwa ya waandaji wakiwemo William Mtitu, Simon Mwakifamba, Zamaradi Mketema pamoja na Shamim (8020 blogspot.com).
Tusikose kwenye uzinduzi huu wa hadhi ya kimataifa ambapo kwa mara ya kwanza jijini Arusha, wageni watapita kwenye REd carpet maalum.
Kiingilio ni Shs 20,000 na Shs 10,000 viti vya kawaida. Na filamu inategemewa kuanza saa 3 kamili usiku katika Ukumbi wa Naura Springs.