Shirikisho la soka duniani FIFA limewapiga marufuku maafisa 3 wa shirikisho la soka la Afrika Kusini kwa tuhuma za kupanga mechi.
Maafisa hao watatu wakiongozwa na aliyekuwa rais wa shirikisho hilo Leslie Sedibe amepigwa marufuku ya miaka 5 na kupigwa faini ya dola elfu $20,245 .
Maafisa wengine waliopigwa marufuku ni Steve Goddard na Adeel Carelse, ambao waliwahi kuwa viongozi wa idara ya waamuzi katika SAFA.
Wawili hao wamepigwa marufuku ya miaka miwili kila mmoja. Kauli hiyo imeafikiwa baada ya uchunguzi wa kina ulioendeshwa na FIFA uliobaini kuwa mechi za kirafiki kabla ya kombe la dunia la mwaka wa 2010 zilipangwa.
Tayari kiongozi mmoja wa magenge ya kupanga mechi raia wa Singapore bwana Wilson Raj Perumal amehukumiwa kifungo kwa makosa hayo.