FFU wa Ngoma Afrika wawasili Berlin!

Wasanii wa kundi la 'FFU'

*Ni kwa kufanya onesho la Sherehe za miaka 50 ya Uhuru

UMOJA wa Watanzania nchini Ujerumani (UTU) unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Desemba 10, 2011 Berlin! Kikosi Kazi cha Ngoma Africa band a.k.a FFU, kimeshatua mjini Berlin kwa kazi ya kutumbuiza katika hafla ya uzinduzi huo. Kikundi hicho cha wasanii kinatarajiwa kushambulia jukwaa kwa burudani murua katika kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania mjini hapa.

Shughuli rasmi zimeanza tangu Desemba 9 na zinaendelea hadi 10, 2011 mjini Berlin ambako ndipo lilipo jengo la Ubalozi wa Tanzania na Mji Mkuu wa Ujerumani. Kwa mujibu wa taarifa zaidi, umoja wa Watanzania unaozinduliwa unatarajia kuwaunganisha Watanzania wote waishio ujerumani, hizi zikiwa ni juhudi za Balozi Ngemera.

Baadhi ya viongozi wa umoja huo ni pamoja na Mfundo Peter Mfundo (Mwenyekiti) na Tullalumba Mloge (Katibu), Sherehe inatarajiwa kufanyika eneo la Apostelkirche 1, 10738 Berlin, UMOJA NI NGUVU WATANZANIA JITOKEZENI ! KUSHREKEA MIAKA 50 YA UHURU! sikiliza muziki at www.ngoma-africa.com