FFU wa Ngoma Africa Band Watoa Heri ya Miaka 51 ya Uhuru!

Kiongozi wa Bendi ya FFU, Kamanda Ras Makunja

BENDI maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya “Ngoma Africa” aka FFU,
inapenda kuwatakia kila la heri na fanaka Watanzania wote kwa kuadhimisha miaka 51
ya Uhuru wa Tanzania. Uongozi wa bendi hiyo unaiombea kila la heri,
Serikali ya Tanzania, Wananchi na Taifa la Tanzania.

Katika kusherekea miaka 51 ya Uhuru, Ngoma Africa Band inawaombea wadau
na wananchi wote popote walipo, kutumia wakati huu kujikomboa kimawazo, na
kuhakikisha kuwa tunajenga na kudumisha umoja, mshikamano na upendo wa
kitaifa ili kuleta maana kamili ya “Uhuru” wa maisha ya Mtanzania.

Katika Kusherekea miaka 51 ya Uhuru, Watanzania tunapaswa zaidi kujenga
na kuziba nyufa zinazo elekea kubomoa au kujaribu kumomonyoa msingi wetu imara
wa umoja, upendo na mshikamano wa kitaifa.

Mungu Ibaraki Tanzania! Mungu Wabariki Watanzania!
Mungi Ibariki Serikali ya Tanzania!

Pata burudani kamili at www.ngoma-africa.com
au http://www.ngoma-africa.com