FFU wa Ngoma Africa Band katika mshike mshike wa usiku usio kwisha!

baadhi ya wanamuziki wa FFU Band wakiwa kazini jukwaani

Heidelberg City, Ujerumani

FFU wa Ngoma Africa band wakiwa kibaruani katika gwaride la usiku usio kwisha! Mjini Heidelberg,Ujerumani,katika onyesho lililofanyika usiku wa jumamosi ya 25.06.2011, ambalo lilikuwa na shamra shamra na kuwadatisha akili wa shabiki, kila mshabiki alidata kiaina yake..kutokana na midundo ya kikosi kazi hiko cha Ngoma Africa band aka FFU.

Mlindimo wa mziki wa bendi hiyo una wanasa washabiki kila kona huko ughaibuni, kunaunguaga shoka na mpini unabaki. www.ngoma-africa.com, vichaa wetu wa mziki FFU walijikuta wakifanya kazi ya ziada jukwaa kwa kupiga masaa matatu zaidi kinyume na mkataba wa masaa 2, hii ilitokana na washabiki sugu kugogewa na muziki ambao uliwadatisha akili kiaina aina.

FFU bado wanaendelea kupereka virungu vya miziki kila kona ughaibuni…usikose kuwachungulia katika FFU Camp at www.ngoma-africa.com