Fernando Santos Apewa Mkataba Mnono hadi 2020

11

Meneja wa sasa wa klabu ya Sunderland Sam Allardyce anatarajiwa kuthibitishwa kuwa Meneja mpya wa Timu ya Taifa ya England .

Bodi ya Chama cha Soka England, kitakaa kumpitisha kama Meneja wao mpya kuchukua nafasi ya Roy Hodgson aliemaliza Mkataba wake Majuzi tu baada ya kwisha Fainali za EURO 2016 na England kutolewa kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na ‘vibonde’ Iceland.

Kwenye mchakato wa uteuzi wa wadhifa huu, Allardyce, maarufu kama Big Sam, alichuana vikali na Meneja wa Hull City Steve Bruce aliewahi kuichezea Manchester United.

Mtendaji Mkuu wa FA, Martin Glenn, alithibitisha kuwa Bodi ya Watu 12 ya FA itajulishwa rasmi kuhusu mchakato wa uteuzi wa Meneja wa Timu ya Taifa ili itoe uamuzi kwenye Kikao chao cha Alhamisi.

Waliopewa mamlaka ya kupendekeza nani atakuwa Mrithi wa Roy Hodgson ni Glenn mwenyewe, Makamu Mwenyekiti wa FA, David Gill, aliewahi kuwa Mtendaji Mkuu wa Man United, na Mkurugenzi wa Ufundi, Dan Ashworth.

Aliewahi kuwa Meneja wa Man United Sir Alex Fergusonaliwaeleza wazi viongozi wa Fa kuwa Mtu pekee anayefaa wadhifa wa Meneja wa England kwa sasa ni Sam Allardyce – BIG SAM.

ureno

Na Chama cha Soka cha Ureno-FPF kimetangaza kumuongeza mkataba kocha Fernando Santos mpaka 2020 baada ya kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo kutwaa taji la michuano ya Ulaya mwaka huu.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 61, ambaye amekuwa akikinoa kikosi hicho toka Septemba mwaka 2014, aliiongoza Ureno kutwaa taji lake la kwanza kubwa la kimataifa pamoja na kucheza bila nyota wake Cristiano Ronaldo katika fainali dhidi ya wenyeji Ufaransa mapema mwezi huu.

Mkataba wake mpya alioongezwa utamfanya kukiongoza kikosi hicho katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na ile ya ijayo ya Ulaya. Santos amewahi kufundisha klabu kubwa nchini Ureno zikiwemo Benfica, Sporting Lisbon na Porto huku pia akiwahi kuinoa timu ya taifa ya Ugiriki.