Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar na Katibu wa TASWA Arusha, Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo Uchaguzi bila vurugu inawezekana na timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira wa pete.
Aidha mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T)Ltd. Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
Awali Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
Kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha vile vile kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo