M
echi za Raundi ya 3 ya Kombe la FA , ambalo kwa sasa linaitwa Emirates FA Cup ambalo huzikutanisha Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la kwanza, Mechi zake zitachezwa mwishoni mwa wiki hii.
Arsenal ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Jumamosi watakuwa Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumapili watakuwa kwao Stamford Bridge kucheza na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
Jumamosi Manchester United watakuwa Old Trafford kucheza na Sheffield United,na Man City watakuwa Ugenini kucheza na Norwich City.
Liverpool wao watafungua dimba Ijumaa wakiwa Ugenini kuivaa Exeter City huku Jumapili Tottenham watawavaa Leicester City ambao wako Nafasi ya Pili katika Msimamo wa Ligi kuu ya England.