Everjobs Tanzania kuwakutanisha Waajiriwa na Waajiri Mtandaoni

Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric Lauer, akiwaelezea waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa jinsi mfumo wao wa tovuti ambao unaweza kuwaunganisha waajiri na waajiriwa kwa urahisi kabisa huku waajiri wakipata nafasi ya kuweza kupata taarifa zote muhimu kutoka kwa wanaoomba kazi kupitia tovuti hiyo pindi wanapokuwa wamejiunga na Kampuni ya Everjobs Tanzania.Mkutano huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric Lauer, akiwaelezea waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa jinsi mfumo wao wa tovuti ambao unaweza kuwaunganisha waajiri na waajiriwa kwa urahisi kabisa huku waajiri wakipata nafasi ya kuweza kupata taarifa zote muhimu kutoka kwa wanaoomba kazi kupitia tovuti hiyo pindi wanapokuwa wamejiunga na Kampuni ya Everjobs Tanzania.Mkutano huo ulifanyika jana katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es salaam.

 Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric Lauer (wa kwanza kushoto) akijibu baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa waliohudhuria mkutano huo hapo jana katika hoteli ya Serena.
 
 Mkurugenzi wa Everjobs Tanzania, Florens Roell akielezea namna ambavyo waajiri na waajiriwa wanaweza kunufaika na Kampuni ya Everjobs Tanzania ambayo inatoa nafasi kwa waajiriwa kuweza kuomba kazi zinazotangazwa kupitia tovuti yao ya www.everjobs.co.tz katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa uliofanyika katika hoteli ya Serena Jijini Dar Es Salaam hapo jana.
 Baadhi ya Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifuatilia maelezo kutoka kwa Wakurugenzi na maafisa wa Everjobs wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa
 
Mkuu wa Kitengo cha Mauzo wa Everjobs Tanzania Lucas Masson (wa pili kulia) akielezea jinsi ya waajiliwa ambavyo wanaweza kujiunga katika tovuti yao ya www.everjobs.co.tz na kuweza kuona nafasi za kazi mbalimbali zinazotangazwa kupitia tovuti hiyo na kuweza kuomba kazi hapo hapo kupitia tovuti.
 Wageni waalikwa wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa kuhusiana na utendaji kazi mzima wa tovuti hiyo 
 Mmoja wa wageni waalikwa akiuliza swali
 Mgeni mwalikwa akiuliza swali 
 Mkurugenzi Mtendaji wa Everjobs Katika Ukanda wa Afrika Eric Lauer akielezea namna Everjob walivyoweza kufikia nchi sita katika bara la Afrika ndani ya muda mfupi huku akieleza changamoto ambazo wanakutana nazo na kuweza kuzitatua, moja ya changamoto wanayokutana nayo ni kwa waaombaji wa nafasi za kazi kudanganya baadhi ya taarifa zao katika wasifu wao kama vile elimu, umri nk.

Dira ya Everjobs 
Dira ya Everjobs ni kurahisisha utafutaji wa kazi na mchakato wa kuajiri kwa kuunganisha wanaotafuta kazi na waajiri kwa haraka sana. Tovuti hii inatoa mwongozo rahisi na unaoeleweka haraka kama vile mbinu za utengenezaji wa CV, namna rahisi ya kutumia tovuti hii, mchujo wa utafutaji wa kiwango cha juu na ushauri wa kitaalamu kuhusu kazi.   
Jukwaa hili linawasaidia mamilioni ya watu kupata fursa sahihi za kazi katika kila hatua ya maisha yao ya kitaaluma. Uorodheshaji wa kazi unaanzia kutoka katika biashara ndogo za ndani mpaka katika makundi makubwa ya makampuni ya kimataifa ya kibiashara. Ikiwa inatoa fursa za kazi kwa vijana walio hitimu pamoja na wataalamu katika uongozi wa ngazi za juu katika biashara.   

Kwa zaidi ya waajiri mia moja tokea siku ya kwanza, Everjobs imefanikiwa kuwapata baadhi ya waajiri wazuri sana tokea ianzishwe na kuwaweka karibu sana na wanao tafuta kazi katika soko la ajira la Tanzania.   
Changamoto ambazo Everjobs wanajaribu kuzitatua 

Watu wanaotafuta nafasi za kazi Tanzania wanakabiliwa na vikwazo vingi, kikwazo cha kwanza kati ya hivyo ni kukosekana kwa uwazi katika soko la ajira. Sio kila mwombaji wa kazi anafahamu fursa sawa za ajira. Madhara yake, wale ambao wana historia  ya kutoka katika familia zenye nafasi nzuri kimaisha  wanapendelewa katika mchakato wa kuajiri, hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa ajira za kujuana na ukabila. Kikwazo cha pili kinahusiana na upendeleo katika kuajiri, iwe inahusiana na  ubaguzi wa kiukabila au kijinsia. Ikiwa inakabiliwa na vikwazo hivi, Everjobs inataka kuwapa watanzania wote nafasi sawa za kuzifikia fursa za ajira.   
www.everjobs.co.tz  8
  
Fursa za ajira kwa Tanzania 
Soko la ajira la Tanzania lina sifa mbali mbali:  Tunaona kukua kwa idadi ya fursa katika eneo la mawasiliano, Huduma za kifedha, ujenzi na NGO’s.  Kwa mujibu wa banki ya dunia (2014), sekta binafsi wanawajibika kwa kutengeneza takribani ajira zote Tanzania, sekta ya umma au serikali inahusika kwa chini ya asilimia tano.  Uwezo wa kuajiwa (kuajirika) ni changamoto ambayo imeelezwa na wasimamizi wakuu katika soko la ajira. Kwa mfano, utafiti uliofanywa na bodi ya vyuo vikuu vya Afrika Mashariki IUCEA. (Inter-University Council for East Africa) mwaka 2014 uligundua kuwa zaidi ya 61% ya vijana nchini Tanzania hawana ujuzi unaoweza kuwawezesha kuajiriwa, utaalamu au ufundi maalumu wanaoufahamu na ujuzi au uwezo mahususi wa msingi unaoendana na kazi.  Kwa mujibu wa benki ya dunia, watu wanaotafuta kazi wapatao 800,000 huingia katika soko la ajira la Tanzania kila mwaka (2014) lakini kwa mujibu wa Wizara ya Fedha ya Tanzania, kulikuwa na nafasi za kazi rasmi 174,000 zilizokuwepo mwaka 2014, jambo ambalo linasababisha wasi wasi  katika soko la ajira.  Katika mwaka huo huo, Banki ya Dunia iliripoti kwamba 12% tu ya nguvu kazi ya Tanzania ina ujuzi wa kati na ujuzi wa juu.  Wakuu wa Idara za Rasilimali watu wanapokea kiasi kikubwa cha CV zilizoandikwa katika karatasi kila siku, jambo ambalo limekuwa ni tatizo na linakosesha ufanisi.  Vile vile wameelezea hatari ya CV ambazo zimegushiwa na umuhimu wa kuwa na huduma kama Everjobs kuweza kukagua uhalisi wa waombaji.     www.everjobs.co.tz  
  
Kuipa teknolojia kipaumbele katika kuajiri mtandaoni 
Ni muhimu kutambua kuwa jukwaa letu halina gharama zozote kwa watahiniwa (waombaji). Utaratibu ni rahisi kabisa: Tengeneza akaunti yako ndani ya dakika chache na omba fursa mbali mbali za kazi zilizopo katika uwanja wetu kupitia www.everjobs.co.tz 

Kwa kufungua akaunti zao, watahiniwa huwa wanaongezwa au kuwekwa katika database yetu ya CV, ambayo huwa inatembelewa na Wakurugenzi wa Rasilimali Watu. Tunawamasisha watu wengi kadri iwezekanavyo kuweka taarifa zao katika tovuti ya Everjobs, hata kama kwa sasa wameajiriwa kwa sababu hii inaweza kukufungulia fursa mpya na kugunduliwa na makampuni ambayo yanaajiri. Kwa hiyo Everjobs inawezesha mabadiliko ya kazi kwa kupitia fursa mpya zinazojitokeza. 

Nia ya kutengeneza Pan African 
Everjobs ina lengo la kuwa taasisi ya kuajiri ya Pan African kwa kuanzisha huduma zake katika nchi 20 kwa wastani na ina fikra hizi mbili:  Kwa wanaotafuta kazi, hii itaweza kupanua upeo wao na kuwapa fursa au nafasi ya kwenda sehemu nyingine kwa kuwapa uwezo wa kuzifikia fursa zilizoko katika nchi nyingine za kiafrika. Kwa mfano, Mtanzania ambaye anataka kupata uzoefu wa kufanya kazi Uganda au Ethiopia wanaweza kufanya hivyo kwa kupitia Everjobs. Kwa maana hiyo Everjobs inachangia katika uhamaji wa vipaji na ujuzi katika nchi za kiafrika.  Kwa waajiri, inapanua wigo wa vipaji na ujuzi katika nchi nyingine, ambazo kimsingi zinakabiliwa na upungufu wa fursa za kazi na ajira katika uchumi wa ndani hivyo kusaidia kufungua fursa hizo katika masoko mengine.     
www.everjobs.co.tz  10
  
Faida zinazoonekana kwa wote 

Kwa wanaotafuta kazi:  
Fursa ya bure ya kuweza kufikia nafasi zote za kazi ambazo zitakuwa zimeorodheshwa na kampuni wanachama/wabia. Uwezo wa kutengeneza taarifa zako bure ambazo zitafanya ujulikane kwa wabia ambao watakuwa wanatafuta mtahitiwa (muombaji) sahihi kutoka katika database yetu ya CV. 

Muunganiko wa moja kwa moja na makampuni kwa sababu maombi ya wale wanaotafuta kazi yatawafikia moja kwa moja Wakurugenzi wa rasilimali watu katika uwanda huu.  UWezo wa kufuatilia maombi yao, wanapewa taarifa moja kwa moja iwapo maombi / CV zao zamechaguliwa au hapana.    

Kwa waajiri  
Waajiri wanakuwa na uhuru wa kuchagua kati ya machaguo mawili: Kuweka tangazo la kazi katika mtandao au kutafuta mtahiniwa wanaomtaka katika database ya CV. Uwezo wa kufikia moja kwa moja kiasi kikubwa cha watahiniwa (wanaoomba kazi) ndani ya Tanzania na jamii ya kiafrika zilizoko ughaibuni iwe huko Ulaya, Amerika ya kaskazini au Asia Kuokoa muda wakati wa kuchagua mtahiniwa anayefaa kupitia katika michujo mingi ya utafutaji (mf. Umri, Elimu, uzoefu wa kazi nk)     
www.everjobs.co.tz  
  
Everjobs katika Afrika 
Everjobs ni portal ya ajira kupitia mtandao ambao tayari unafanya kazi zake katika nchi za Cameroon, Ivory Coast, Senegal, Uganda na Ethiopia. Imezinduliwa hapa Afrika Machi mwaka 2015 na inaongozwa na Mwanzilishi mwenza na Mkurugenzi wa Afrika, Eric Lauer, Everjobs ina lengo la kuwa ni uwanja wa kutegemewa wa kuajiri katika nchi za Pan-Afrika. Kampuni hii inadhaminiwa na Africa Internet Group (AIG).