Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza na kikundi cha akinamama kinachotengeneza vikoi na bidhaa mbalimbali mjini Ifakara. Kikundi hicho kimewezeshwa na EU na Umoja wa Mataifa UN.
Akinamama wa kikundi cha utengenezaji vikoi na bidhaa nyingine za nguo wakiendesha moja ya mashine yao rahisi kutengeneza nguo hizo. Balozi Filiberto Sebregondi na Alvaro Rodriguez walitembelea miradi mbalimbali inayofadhiliwa na taasisi hizo.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez wakisaidiana kuendesha moja ya mashine rahisi za ufumaji vitambaa eneo la Ifakara, mkoani Morogoro.
Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akiendesha moja ya mashine rahisi kuandaa vitambaa.
Mmoja wa akinamama wa kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali akimpongeza Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi mara baada ya kupewa zawadi ya vitambaa na umoja wa akinamama alipotembelea mradi wao.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi (wa kwanza kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipata maelezo kutoka katika kikundi hicho cha uvumaji na uandaaji vitambaa.
Baadhi ya vitambaa na bidhaa zilizoandaliwa na kikundi cha ufumaji na kudarizi vitambaa mbalimbali Mjini la Ifakara, mkoani Morogoro.
Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi akizungumza katika moja ya vituo vya radio jamii Ifakara.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiuliza maswali kwenye moja ya vituo vya radio za jamii Ifakara jana.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Filiberto Sebregondi wakiwa katika kituo cha Redio Pambazuko Mjini Ifakara walipotembelea radio za kijamii na kujua namna zinazofanya kazi kwa jamii.