Mwamuzi wa pambano la ngumi la wacheza filamu maarufu Tanzania kati ya Wema Sepetu na Jacklen Wolper, John Chagu akiwainua mikono juu mabondia Wolper (kushoto) na Sepetu (kulia) kuashiria mpambano wao ni ngoma droo. Picha na Blog ya Super ‘D’.
Bondia Wema Sepetu akimkimbia mpinzani wake, Jacklen Wolper wakati wa mpambano wao baada ya masumbwi kufululiza hata hivyo mpambano huo ulimalizika bila mbabe.
Mabondia wacheza filamu nchini Wema Sepetu (kushoto) na Jacklen Wolper (kulia) wakiwa katika picha ya pozi baada ya pambano lao.