Edward Lowassa atembelea Banda la Wizara ya Fedha Sabasaba


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akimsikiliza Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma katika Banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.


Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akisaini kitabu cha wageni huku akishuhudiwa na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma kwenye Banda la Wizara ya Fedha Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.

Waziri Mkuu mstaafu John Malecela, akisaini kitabu cha Wageni huku akishuhudiwa na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma kwenye Banda la Wizara ya Fedha Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.


Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania, John Malecela, akizungumza na Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma kwenye Banda la Wizara hiyo kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yanayofanyika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.


Ofisa Habari na Mawasiliano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Doreen Makaya akimwonesha Kitabu cha Idadi ya Sensa ya Mwaka 2007, Edward Lowassa akiambatana na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo (kulia) ndani ya Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Viwanja vya Julius K. Nyerere Dar es Salaam jana.


Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta wa Wizara Fedha, Elimu Sekeni akitoa ufafanuzi kuhusiana na majukumu ya Idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Fedha wizarani kwa Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa kwenye Banda la Wizara ya Fedha katika Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara Viwanja vya Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.


Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akipata maelezo kwa kutoka kwa Ofisa Huduma kwa Mlipa Kodi (TRA) kwenye Banda la Wizara ya Fedha kwenye Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.


Mkuu wa Idara ya Masomo ya Biashara na Uongozi na Masomo ya jioni wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Adolf Mwakinyuke akimweleza maendeleo ya Chuo hicho, Edward Lowassa kwenye Banda la Wizara ya Fedha, Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere jijini Dar es Salaam jana.