EABL Yaalika Udhamini kwa Wanachuo

Nembo ya kampuni ya EABL

KAMPUNI ya EABL imeanza kupokea maombi ya wanafunzi wanaotaka kudhaminiwa kwa masomo ya elimu ya juu (Chuo Kikuu), ikiwa ni moja ya mchango wake ya kurudisha faida katika jamii inayoiwezesha kampuni hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kampuni hiyo Oktoba 23, wanafunzi wanaohitaji kupata udhamini huo watatakiwa kujaza fomu maalumu (imeambatanishwa chini ya habari hii) na kuambatanisha nakala ya cheti cha kidato cha nne na sita pamoja na barua ya uthibitisho, fomu ya maombi iliyojazwa.

Aidha muombaji anatakiwa pia kuambatanisha barua ya kuitwa kwenye masomo ya chuo, lakini ambao hawajaitwa chuo watatakiwa kuwasilisha barua hiyo kabla ya kupewa udhamini, maombi hayo ni lazima yaambatanishwe na uthibitisho kwamba muombaji hana uwezo wa kujisomesha kifedha.

Taarifa zaidi katika ufafanuzi wa ufadhili huo EABL watagharamia kila kitu kwa watakao shinda ufadhili huo ikiwa ni pamoja na karo, malazi, fedha ya kujikimu kwa kila mwezi katika michepuo ifuatayo;- Shahada ya Biashara, Shahada ya Uhandisi, Shahada ya Sayansi ya Chakula, Shahada ya Biashara/Teknolojia ya Mawasiliano/ Sayansi ya Kompyuta.

Famu za maombi pia zinapatikana katika tovuti ya www.eablfoundation.com
Fomu ya Ufadhili wa Masomo-English
Fomu ya ufadhili wa masomo-Swahili