Duu! Kweli Van Gaal Ana Roho Ngumu, Hebu Soma Hii Habari

Louis-van-Gaal

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema njia rahisi sasa kwa klabu hiyo kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao ni kushinda Europa League.

Manchester United walishindwa 2-1 ugenini Sunderland Jumamosi na sasa wamo alama sita nyuma ya klabu nne zinazoongoza Ligi kuu ya Uingereza.

Tangu msimu uliopita, washindi wa Europa League wamekuwa wakizawadiwa nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya wakiingia hatua ya kufuzu kabla ya hatua ya makundi au hatua ya makundi.

Van Gaal hata hivyo amesema hajapoteza matumaini ya kumaliza katika nne bora ligini. United watacheza mechi ya mkumbo wa kwanza Europa League hatua ya 32 bora dhidi ya klabu ya Denmark FC Midtjylland Alhamisi.

Watakutana na Shrewsbury katika Kombe la FA wikendi ijayo. Mechi yao ijayo Ligi ya Kuu ya Uingereza itakuwa tarehe 28 Februari dhidi ya Arsenal uwanjani Old Trafford