Na Ronald Ndungi, EANA-Arusha
DUKA Kuu la Uchumi wa Kenya limejipanga kujitanua katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Afisa Mtendaji Mkuu wa Duka hilo, alisema mwishoni mwa wiki.
Ofisa huyo, Jonathan Ciano alisema fedha za kufanya upanuzi huo zitapatikana Machi mwaka huu.
“Tunataka kujitanua katika nchi zote wanachama wa EAC ili kunufaika na uwezo wa manunuzi unaoendelea kukua katika kanda hii,” Ciano alisema katika hafla ya kumpata msindi wa shindano la Mteja wa Uchumi. Aliongeza kuwa duka hilo kuu lina maduka mengine madomadogo 32 katika kanda ya EAC. Kwa hivi sasa ina maduka 26 nchini Kenya, Uganda 5 na Tanzania duka moja.
“Tuna mpango wa kufungua duka lingine nchini Tanzania na hivi sasa tunafanya majadiliano na mwekezaji wa kutupatia eneo,” alisema.
Mipango mingine ya duka hilo ni pamoja na kufungua matawi yake nchini Rwanda na Sudani Kusini.