Mkuu wa kituo cha Kulelea Watoto yatima cha Al-Madina, Bi. Kulthum Juma akizungumzia kuhusu kituo hicho pamoja na kutoa shukrani kwa kampuni ya Multichoice Tanzania kwa kuendelea kukisaidia kituo cha hicho ambacho kina takribani watoto 68 na pia kituo hicho kipo eneo la Tandale kwa Tumbo jijini Dar.
Ustadhi Mashaka Salim akitoa neno.
Mkurugenzi wa Multichoice Tanzania, Peter Fauel akichukua chakula wakati wa kuwafuturisha watoto yatima wanaolelewa katika kituo cha Al-Madina kilichopo Tandale kwa Tumbo, Wa pili kutoka kulia ni Meneja uendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Shelukindo.
Meneja Uhusiano wa Kampuni ya Multichoice Tanzania, Barbara Kambogi, akitoa huduma ya chakula kwa watoto yatima hii ikiwa ni njia mojawapo ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Baadhi ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakichukua chakula katika futari iliyoandaliwa na kampuni ya Multichoice Tanzania.
Baadhi ya Watoto yatima, Wafanyakazi wa Multichoice Tanzania pamoja na viongozi wa kituo hicho cha Al-Madina wakijumuika katika futari hii ikiwa ni moja wapo ya kutoa msaada katika vituo mbalimbali hapa nchini.
Meneja wa Fedha wa Multichoice Tanzania, Francis Senguji akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kampuni ya Multichoice Tanzania kwa waliofika na kujumuika nao katika futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Multichoice Tanzania.