Dk Shein azungumza na kikosi kazi kilichoshughulikia zao la karafuu

Rais wa Mapinduzi Zanzibar akisalimiana na viongozi

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Viongozi wa Vikosi vya Ulinzi ambao
ni Wajumbe wa Kikosi cha (Task Force), ya Taifa kuhusu uvunaji wa zao
la karafuu,alipowasili katika viwanja vya ukumbi wa Kiwanda cha
Makonyo Wawi Pemba akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba
jana.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Naibu Waziri Viwanda na Masoko akimkabidhi Mhe. Rais tuzo

Naibu Waziri wa Biashara,Viwanda na Masoko Thuwaiba
Edington Kisasi,akimkabidhi zawadi Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,ya tunzo ya karafuu ya mwaka
2011-2012,katika mkutano wa ufungaji wa msimu wa zao la Karafuu,hafla
hiyo ilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kiwanda cha Makonyo Wawi
Pemba.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kikosi kazi

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein,akizungumza na Kikosi kazi cha (Task Force) ya Taifa
kilichoshuhulikia uvunaji na uuzwaji wa zao la karafuu,katika ukumbi
wa Kiwanda cha Makonyo Wawi Pemba,Rais aliufunga Msimu wa zao hilo
kwa mwaka 2011-2012 jana,akiwa katika ziara ya Mkoa wa Kusini Pemba
.[Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]

Mh. Rais wa Zanzibar akipiga picha ya Pamoja na kikosi kazi

Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk
Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Kikosi kazi (Task
Force) ya taifa kuhusu uvunaji wa zao la karafuu huko kiwanda cha
Makonyo Wawi ,Wilaya ya Chakechake Pemba , akiwa katika ziara ya Mkoa
wa Kusini Pemba jana. [Picha na Ramadhan Othman,Pemba.]