Meza Kuu, kuanzia kushoto ni Mratibu Mkuu wa FASDO nchini, Joyce Msigwa,
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa
Kituo cha Utamaduni cha Urusi nchini, Alexander Tsykunov na mwisho ni
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande.
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa
Kituo cha Utamaduni cha Urusi nchini, Alexander Tsykunov na mwisho ni
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande.
Mkurugenzi Mtendaji wa FASDO, Tedvan Chande akizungumza jambo wakati wa sherehe hizo
Mratibu wa shindano hilo, Joyce Msigwa akizungumza jambo.
Mshereheshaji wa sherehe hizo ambaye pia ni Mratibu Msaidizi, Tunukiwa Daudi akifafanua jambo.
Mzee Nabora Akizungumza Jambo wakati wa Sherehe hizo
Baadhi ya washindi wakiwa wanakabidhiwa zawadi zao
Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa akitazama baadhi ya kazi ambazo wamefanya vijana hao.
Burudani ya sanaa ikiendelea.
Baadhi ya washiriki wachoraji wakiendelea na Mafunzo
Kushoto ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe ambaye pia ni mbunifu mavazi akitoa somo kwa baadhi ya washiriki
Mmoja ya washiriki akiwa anaendelea kuchora wakati wa Sherehe hizo
Picha ya Pamoja.
Shirika la FASDO (Faru Arts and Sports Develepment Organization) limetoa zawadi
kwa washindi wa shindano la Na Mimi Nipo- Online Arts and Science Competition
katika ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi nchini (Russian Tanzania Cultural Center).
kwa washindi wa shindano la Na Mimi Nipo- Online Arts and Science Competition
katika ukumbi wa kituo cha utamaduni cha Urusi nchini (Russian Tanzania Cultural Center).
Shindano hilo lililofanyika jana lilihusisha vipaji vya uchoraji, sanaa za mikono na ubunifu wa kisayansi lililozinduliwa mwezi Februari mwaka huu kwa lengo la kutambua vipaji vya vijana
wenye umri kati ya miaka 12 hadi 24 limefikia kilele chake leo hii kwa kuwapata
washindi sita, wawiliwawili kutoka katika fani za Uchoraji, Sanaa za Mikono na
Ubunifu wa Kisayansi.
wenye umri kati ya miaka 12 hadi 24 limefikia kilele chake leo hii kwa kuwapata
washindi sita, wawiliwawili kutoka katika fani za Uchoraji, Sanaa za Mikono na
Ubunifu wa Kisayansi.
Zoezi la kutoa zawadi kwa washindi hao lilihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini
Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi
nchini hapa, Alexander Tsykunov na wageni waalikwa.
Ubelgiji, Dr. Diodorus Buberwa, Mkurugenzi wa Kituo cha utamaduni cha Urusi
nchini hapa, Alexander Tsykunov na wageni waalikwa.
Akizungumza na washiriki pamoja na wageni waalikwa katika Sherehe hizo Balozi wa Tanzania Nchini Ubelgiji aliwapongeza sana vijana kwa kuwa na vipaji vya hali ya juu na kusisitiza kuwa eneo hili la sanaa ya Uchoraji linatakiwa kupewa kipaumbele, aliongeza kuwa Tanzania sasa inatakiwa kuwa na maeneo zaidi kwa ajili ya kukuza sanaa hizi, na katika kuendeleza na kusapoti sanaa , Mh. Balozi Buberwa amechangia Tsh 1,000,000.
Washiriki walikuwa 27 lakini waliopata zawadi walikuwa ni washiriki 6 ambao walizingatia umri kati ya miaka 12 hadi 24 na washindi hao ni pamoja na Thomas Mwakilima, Anhony Tendwa, Primus Mapunda, Philipo Frolian, Cornelio Malya na Anderson Msangi washindi wote wamepata zawadi Dola 300.