DoubleTree Hoteli Yaendeleza Kampeni ya nishati ya Mwanga wa Jua yagawa taa 200 Mtwara

DSC_0059

Mkurugenzi wa Kanda wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton ya Dar es Salaam Bw. Judd Lehmann (kulia) akikabidhi moja ya taa ya Umeme Jua kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba mkoani Mtwara. Anayeshuhudia tukio hilo ni Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia (katikati).

DSC_0051

Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata akimkabidhi Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia (katikati) aina ya taa zinazitumia Nishati ya Jua huku mtoto wa shule msingi Dihimba akishiriki kupokea taa hiyo.

DSC_0049

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Mh. Hawa Ghasia akimkabidhi taa ya Umeme Jua mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba.

DSC_0038

Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya DoubleTree by Hilton Bw. Florenso Kirambata akitoa mafunzo ya matumizi ya taa hizo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba mkoani Mtwara.

DSC_0017

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Dihimba wakati wa hafla ya kukabidhiwa taa za Umeme wa Nishati mbadala zilizotolewa na Hoteli ya Double Tree.

Hoteli ya Double Tree by Hilton ya jijini Dar es Salaam imeendelea na kampeni zake kabambe ya matumizi ya nishati ya jua kwa kugawa taa 200 kwenye shule ya Msingi Dihimba kata ya Dihimba wilaya ya Mtwara vijijini Mkoani wa Mtwara, Moblog linaripoti.

Akizungumza kwenye hafla hiyo fupi ya kugawa taa hizo, Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu, Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa (Tamisemi) Hawa Ghasia amesema kwamba msaada huo wa Double Tree kwa shule hiyo ni kielelezo tosha kwamba sekta binafsi zina mchango mkubwa katika sekta ya elimu hapa nchini.

“Napenda kuchukua fursa hii adhimu kuwashukuru uongozi na wafanyakazi wote wa Double Tree kwa msaada wao mkubwa kwa shule yetu ya hapa Dihimba ambapo watoto wetu watasoma katika mazingira rafiki yatayowawezesha kufaulu mitihani yao,’ amesema Ghasia.

Waziri Ghasia amesema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabia nchi Serikali, wananchi na wadau wote wa maendeleo hawawezi kuendelea kutegemea umeme wa vyanzo vya maji na badala yake umeme wa jua ambao ni nishati mbadala ni ufumbuzi wa tatizo la nishati nchini.

Amesema mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya nchi hasa kwenye nishati ni muhimu kwa sababu ni nishati ndio injini ya Uchumi wa taifa lolote lile hapa duniani kwa sasa.

‘lakini kampeni hizi zitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi kutambua na kuelewa nishati mbadala na umuhimu wake katika maisha ya kila siku ikiwemo mazingira,” alisisitiza

Hoteli ya DoubleTree ilizindua rasmi kampeni ya matumizi ya nishati ya jua ambayo itadumu kwa muda wa miaka miwili katika shule za msingi nchi nzima miezi kadhaa iliyopita.

DoubleTree itakuwa ikigawa taa 200 za mezani zenye kutumia nishati ya jua kwa wanafunzi wa darasa la saba kwa shule tofauti kila mwezi, lengo likiwa nikuwafanya wawe na ufahamu zaidi juu ya chanzo kingine cha umeme ambacho ni rafiki wa mazingira kwa kupitia mafunzo katika madarasa yao.

Katika kata ya Dihimba ina jumla ya wanafunzi wa shule za msingi wavulana 654 na wasichana 645 jumla yao ni 1299. Shule ya msingi Dihimba imepata mafanikio ya kielimu kwa mwaka 2012/2013 kwa kushika nafasi ya nne kati ya kata 28 katika mtihani wa taifa wa darasa la saba mwaka jana.

Katika matokeo hayo shule ya msingi Dihimba ilishika nafasi ya nne kati ya shule 98 kiwilaya na mafanikio mengine ni kuandikisha wavulana 135 na wasichana 126 katika kujiunga na darasa la kwanza mwaka huu.