Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) akitoa risala yake kwenye hafla ya kukabidhi Taa 200 za Nishati ya Jua kwa Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande ikiwa ni mwendelezo ya kampeni iliyozinduliwa na Hoteli ya DoubleTree By Hilton jijini Dar kwa wanafunzi wa shule za msingi ambapo ameipongeza hoteli hiyo kwa kubuni kampeni kama hiyo kwani Taa hizo ni rafiki wa mazingira kwa kuwa zinatumia Nishati ya Jua zitawasaidia wanafunzi kujisomea na familia zao pia kupata Mwanga kunapokuwa tatizo la kukatika kwa Umeme na pia itaongeza ufaulu kwa Wanafunzi kwa sababu watakuwa wanauwezo wa kujisomea nyakati za usiku.
Aidha amewaasa wanafunzi hao kuzitunza taa hizo na kuzitumia kwa maelngo yaliyokusudiwa. Kushoto ni Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk pamoja na Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (wa pili kulia).
Mkurugenzi wa Mauzo wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Florenso Kirambata (katikati) akitoa maelezo ya jinsi ya kutumia taa ndogo za mezani zinazotumia Nishati ya Jua na umuhimu wake tofauti na kutumia Mafuta ya Taa kwa Wanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi ya Mji Mpya wakati uongozi wa hoteli hiyo ulipotembelea shule hiyo iliyopo Mabwepande kwa nia ya kuendesha mafunzo na kugawa Taa 200 bure kwa Wanafunzi hao. Kushoto ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mh. Angellah Kairuki (Mb) na Kulia ni Meneja Mkuu wa Hoteli ya Double Tree by Hilton Rode Perk.
Mwenyekiti wa bodi ya Shule hiyo Epimack Vinivuni akitoa shukrani kwa uongozi wa hoteli ya Double Tree by Hilton kwa kuwa na mkakati madhubuti wa kuwaelimisha vijana umuhimu wa matumizi ya Umeme mbadala wa Nishati ya Jua ambao ni rafiki wa mazingira.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mji Mpya, Davis Mkaruka akizungumza baada ya mafunzo yaliyolewa na Double Tree by Hilton kwa wanafunzi wa darasa la saba akisema ilikuwa ni njia nzuri ya kuwaelimisha watoto juu ya nishati ya jua na kuwa wamefurahi kupewa bure taa ndogo za mezani ambazo ni rahisi kutumia na zina faida nyingi kwao na familia zao.
Wanafunzo hao wakifurahia Taa ndogo la ‘Solar Energy’ walizopewa. Nyuma ni Bw. Florenso Kirambata na Meneja Mkuu wa hoteli ya Double Tree by Hilton Hotel Rode Perk.
Hoteli ya Double Tree by Hilton Dar es Salaam leo imefanya ziara katika Shule ya Msingi Mji Mpya iliyopo Mabwepande kwa lengo la kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wa darasa la saba kuhusu umuhimu wa umeme wa nishati ya jua.
Mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Double Tree by Hilton wa miaka miwili wa kuwakufahamisha na kuwashirikisha wanafunzi juu ya faida za nishati ya jua tofauti na matumizi ya mafuta ya taa, kuni na vyanzo vingine vya mwanga ambavyo vina madhara kwa mazingira, afya na vifaa vya nyumbani.
Katika ziara hiyo shule hapo Hoteli ya Double Tree by Hiltonimegawa kwa wanafunzi hao taa ndogo za mezani 200 zinazotumia nishati ya jua, ambazo wanafunzi hao wamekwenda nazo majumbani kwao kuzitumia kusomea usiku kwa faida yao na familia yao.