Dk. Samuel M. Nyantahe
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemteua Dk. Samuel M. Nyantahe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC). Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Uteuzi huu umeanza tarehe 20 Julai, 2016.
Kabla ya uteuzi huo Dk. Samuel M. Nyantahe alikuwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI).
Dk. Samuel M. Nyantahe anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya ambaye amejiuzulu wadhifa huo.
Imetolewa na; Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma, 25 Julai, 2016