Dkt. Bilal Azindua Uwanja wa Ndege Mpanda

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, wakati wa hafla ya uzinduzi wa uwanja huo iliyofanyika mkoa Mpya wa Katavi, Nov 24, 2012 katika uwanja huo baada ya kukamilika kwa ukarabati uliogharimu kiasi cha Sh. Bilioni 30. Kulia ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, (kushoto) ni Mama Zakhia Bilal (wa pili kushoto) ni Katibu Mkuu wa Miundombinu, Omar Chombo na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt.Charles Tizeba. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mkewe Mama Zakhia Bilal, wakifurahia ngoma ya asili ya kikundi cha sanaa cha Mama Monica, chenye maskani yake, Maji Moto Mpanda mjini, wakati walipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Mpanda, Nov 24, 2012 kwa ajili ya kuzindua rasmi uwanja huo na Mkoa wa Katavi

Mbunge mstaafu, Chrisant Mzindakaya, akijumuika na wasanii wa ngoza ya asili kucheza ngoma ya kabila la Wakonongo wa Inyonga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Uwanja wa Ndege wa Mpanda, uliofanyika sambamba na uzinduzi wa mkoa mpya wa Katavi. Picha na OMR