Dkt Bilal Aendesha Kikao cha Muungano Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiendesha Kikao cha Muungano, kilichofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar leo, Januari 14, 2013. Wa pili (kushoto) ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (wa pili (kulia) Ni Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd (kushoto) ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samiah Suluhu na (kulia) ni Waziri wa nchi Ofsi ya Makamu wa pili wa Rais zanzibar,

Baadhi ya Mawaziri wakiwa ukumbini humo wakati wakifuatilia kikao hicho cha Muumgano kilichoendeshwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, (hayupo pichani), leo katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Samiah Suluhu, mara baada ya kumalizika kwa kikao cha Muungano, kilichofanyika leo Januari 14, 2013 katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort, mjini Zanzibar. Picha na OMR