KATIBU Mkuu mteule wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dk. Vincent Mashingi mwenye umri wa miaka 43 ameteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freeman Mbowe. Dk. Mashingi ambaye rasmi atashika nafasi ya Dk. Peter Slaa aliyejiengua ndani ya Chadema inadaiwa huenda akawa ndiye Katibu Mkuu wa chama cha siasa msomi zaidi duniani.
JINA: Dr. Vincent Mashingi
UMRI: Miaka 43
KABILA: Msukuma
TAALUMA: Daktari Bingwa wa Binadamu (MMED) na Daktari wa Falsafa (PhD).
ELIMU:
1981 – 1987 Elimu ya Msingi (Shule ya msingi Iligamba)
1988 – 1992 Elimu ya Sekondari (St.Pius seminary)
1992 – 1994 A-Level PCB (Mzumbe High School).
1995 – 2001 Chuo Kikuu cha Makerere (Degree ya Udaktari MD)
2003 – 2005 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Shahada ya pili – udaktari bingwa (MMED Anaesthesiology).
2004 – 2004 Chuo Kikuu Kishiriki Muhimbili (Astashahada ya Utafiti)
2008 – 2010 Evin School of Management (Shahada ya Uzamili (Masters) ya Public Relations (CSR)
2007 – 2010 Blekinge Institute of Technology (Shahada ya pili (Masters) ya Usimamizi wa biashara, MBA)
2010-2010
University of Carlifonia – Anderson School (Stashahada ya Management Development)
2008 – 2008 University of Maryland School of Medicine (Astashahada Human Virology)
2010 – 2016 Chuo Kikuu Huria Tanzania (Shahada ya uzamivu (PHD) ya Uongozi.
UZOEFU WA KITAALUMA,
2001 2002, Daktari wa mazoezi – Intern doctor (Hospitali ya taifa Muhimbili).
2002 – 2003, Mtafiti wa kujitegemea (Freelance Researcher).
2003 – 2005, Daktari (Hospitali ya Taifa Muhimbili)
2005 – 2006, Daktari bingwa (Hospitali ya Regency).
2006 – 2008, Msimamizi wa mradi (Shirika la kimataifa la afya IMA World Health)
2008 – 2016, Mshauri wa tiba (TB and HIV), Shirika la afya la Kimataifa la IMA WorldHealth.
Kwa kifupi Dk. Vincent Mashingi ana degree 1, Masters 3, Certificate 2, Diploma 1 na PhD 1.