Dk. Tulia Ackson Mwansasu, Naibu Spika wa Bunge la Tanzania.
BUNGE la Tanzania limemchaguwa Mbunge wa Kuteuliwa na Rais Dk. Tulia Ackson Mwansasu kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dk. Tulia Mwansasu amechaguliwa katika nafasi hiyo baada ya kumshinda mgombea mwenzake wa nafasi hiyo, Magdalena Sakaya toka Chama cha Wananchi CUF aliyekuwa mgombea kwenye nafasi hiyo.
Dk. Tulia Mwansasu ameshinda nafasi hiyo baada ya kupata jumla ya kura 250 ikiwa ni sawa na asilimia 71.2 ya kura zote 351 zilizopigwa na wabunge kwenye zoezi la upigaji kura. Mpinzani wake Magdalena Sakaya ameambulia kura 101 ikiwa ni sawa na asilimia 28.8.