Dk. Shein: Serikali yangu itafanya mapinduzi ya kilimo

Mwandishi Wetu
Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein amesema

Serikali ya Awamu ya Saba imepanga kufanya Mapinduzi ya Kilimo ikiwa ni pamoja na kuwasaidia

wakulima wadogowadogo hasa hata wale mazao yao yanayoathiriwa na jua la kiangazi.

Dk. Shein amesema hayo jana mjini Kengeja Kwajibwa, Mkoa wa Kusini Pemba wakati alipokuwa

akizungumza na wakulima wa bonde hilo ambao mazao yao yameathirika kwa jua.

Alisema kuwa serikali imejiandaa kiasi kikubwa katika kuhakikisha wakulima walioathirika

kutokana na jua wanasaidiwa hasa kupewa msaada wa mbegu za nafaka.

Alisema kuwa miongoni mwa juhudi zinazochukuliwa na serikali ni pamoja na kuimarisha kilimo

cha umwagiliaji mbapo tayari miundombinu yake imewekwa, alisema kuwa hekta 800 zitaandaliwa

kwa ajili hiyo.

Dk. Shein alisema kuwa miogoni mwa juhudi zlizoandaliwa na serikali katika kuimarisha mazao

ya kilimo ni pamoja na kuimarisha kilimo cha muhogo kwa kuanza kufanya utafiti juu ya zao

hilo kwa kuwashirikisha wataalamu toka taasisi ya COTECH ya Dar-es-Salaam.

Alielza kuwa taasisi hiyo inayoshughilikia utafiti hasa wa mbegu za kilimo, itasaidia kwa

kiasi kikubwa kuratibu tafiti za mazao ya kilimo likiwemo zao la muhogo ambalo ni zao muhimu

sana na tayari nchi nyingi wameweza kusarifu aina mbalimbali za vyakula vikiwemo mikate na

tambi.

Katika malezo yake, Dk. Shein alisema hatua zinazochukuliwa kuimarisha sekta ya kilimo ni

pamoja na kubadilisha matumizi ya zao la muhogo na matunda yakiwemo maembe.

“lengo ni kuleta mbegu za maembe za miaka minne ambazo tayari kwa baadhi ya maeneo ya

Tanzania Bara hasa katika eneo la Mkoa wa Pwani wamekuwa wakilima na wameanza kuvuna…hata

hivyo maembe ya asili hayataachwa kwani nayo yana umuhimu wake,” alisema

Naye Ofisa wa Kilimo Mkoa wa Kusini Pemba, Ali Mohammed Omar, alimueleza Dk. Shein kuwa

Wizara ya kilimo imeandaa mikakati madhubuti ya kuwasaidia wakulima kupata mbegu ambazo

zinastahamili ukame, kuwahimiza kupanda mazao ya muda mfupi na pembejeo.