Dk. Shein, Balozi wa Japan Wazinduwa Mradi wa Uhimarishaji Umeme

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Balozi wa Japan nchini Tanzania Masaki Okada. kwa pamoja wakikata utepe kuzindua mradi wa uimarishaji Miundombinu ya Usambazaji Umeme Zanzibar, katika hafla iliyofanyika leo Mtoni Kituo Kikuu cha Umeme, Wilaya ya Magharibi Unguja.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Baadhi ya mafundi na wafanyakazi wa Shirika la Umeme la Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, alipozungumza katika sherehe za uzinduzi wa mradi wa uimarishaji Miundombinu ya Usambazaji Umeme Zanzibar, katika hafla iliyofanyika Mtoni Kituo Kikuu cha Umeme, Wilaya ya Magharibi Unguja.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, (katikati) na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif, wakifuatana wakati uzinduzi wa mradi wa uimarishaji Miundombinu ya Usambazaji Umeme Zanzibar, katika hafla iliyofanyika Mtoni Kituo Kikuu cha Umeme, Wilaya ya Magharibi Unguja.[Picha na Ramadhan Othman, Ikulu.]