Dk Shein Azungumza na Viongozi wa CCM Ofisi Kuu Kisiwandui

Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisisitiza jambo alipokua akizungumza na Viongozi wa Tawi la CCM Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui, wakiwemo Viongozi wa Jumuiya mbalimbali za Chama hicho katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar jana, Makamo Mwenyekiti alifanya ziara maalum ya kusalimiana na Viongozi hao ikiwa ni pamoja na kuimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) (kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai. [Picha na Ramadhan Othman, Ikulu]